Ibadhi.com

3. SIFA ZA LAZIMA KWA ALLAH MTUKUFU

Kwa hakika Allah mtukufu -peke yake- ndiye mwenye kusifika kidhati kwa sifa zifuatazo: Kuwepo, Utangu, Kubakia, Uhai, Kutaka, Uwezo, Elimu, Usikivu, Uoni, Kutosheka (Ukwasi), Upweke, Kutofautiana na vyote vyenye kutokeza (viumbe).

Basi:

 1. Yeye Allah mtukufu yupo.
 2. Yeye Allah mtukufu ni wa tangu (hana mwanzo).
 3. Yeye Allah mtukufu ni mwenye kubaki (hana mwisho).
 4. Yeye Allah mtukufu ni hai.
 5. Yeye Allah mtukufu ni mwenye kutaka.
 6. Yeye Allah mtukufu ni mwenye uwezo.
 7. Yeye Allah mtukufu ni mwenye kujua.
 8. Yeye Allah mtukufu ni mwenye kusikia.
 9. Yeye Allah mtukufu ni mwenye kuona.
 10. Yeye Allah mtukufu ni mmoja.
 11. Yeye Allah mtukufu ni mkwasi (asiyehitaji).
 12. Yeye Allah mtukufu yuko tafauti na viumbe wote.

Tujuwe kuwa kusifika Allah mtukufu kwa sifa hizi sio kwa njia ya kutegemea sifa wala kuhitajia sifa; kwani Allah mtukufu hajapangika wala si mwenye kufikiwa na upungufu wowote; basi kusifika Allah mtukufu kwa sifa hizi ni kwa njia ya kuujuwa ukamilifu wake wa kidhati na utukufu wake wa kidhati, basi sifa hizo sio vitu vyengine visivyokuwa dhati yake Allah mtukufu, lakini ni kumtakasa Allah mtukufu na kila lililo kinyume na sifa hizo, tujuwe kuwa Allah mtukufu hana mfano wa kufanana na chengine chochote wala hakuna chenye mfano wa kufanana na yeye.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment