Ibadhi.com

2. KUTOMFIKIRI ALLAH MTUKUFU

 Allah mtukufu ni mkamilifu wa kidhati, yeye ni Mkwasi asiyehitaji, basi kwepo viumbe na kukosekana kwa viumbe hakuathiri chochote katika dhati ya Muumba ambaye ni Allah mtukufu; kwani yeye amevitangulia viumbe vyake, alikuwepo wala hakukuwa na chengine chochote isipokuwa yeye peke yake, sehemu na wakati na vilivyomo katika sehemu na kupitiwa na wakati vyote ni viumbe vyake Allah mtukufu, yeye si mwenye kubadilika; kwani badiliko ni hali mpya isiyokuwepo kabla; kwa hiyo badiliko ni kiumbe, basi tujuwe kuwa Allah mtukufu hana mfano wowote, na haiwezekani kuwa yeye na mfano wa chochote, tunamjua Allah mtukufu kwa dalili za vitendo vyake, na sio kwa kumfikiri na kumjengea sura, ametakasika Allah mtukufu na uwezekano wa kuwa na sura au kuingia katika fikra ya kiumbe chochote.

Hakika sisi hatuna uwezo wa kumfikiri Allah mtukufu, kwa sababu hatuna uwezo wa kufikiri kitu chochote kilichoko nje ya kudhibitiwa na na mipaka ya sehemu, wakati, kiza na nuru, na vyote hivo ni viumbe Allah mtukufu ameviumba, yeye yupo kabla ya kupatikana chochote katika hivyo, na yeye habadiliki, kwa sababu kubadilika ni pitio la kupatikana hali baada ya kukosekana hali, na kwa hiyo badiliko ni kiumbe, basi badiliko ni sifa ya viumbe peke yao, na kila kinachobadilika bila shaka ni kuimbe, basi Allah mtukufu ametakasika na sifa ya kubadilika.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment