Ibadhi.com

30. KUHUSU MACHO (العين)

 

874. Ama kuhusu kauli inayosema:

{وَلِتُصْنَعَ عَلَى عَيْنِي}[1]

Maana yake, "{Na ili ulelewe machoni mwangu}".

Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Na ili ulelewe kwa amri Yangu”.

L-Hasan kasema, "Na ili ulelewe kwa ujuzi Wangu”. Na Mujahiid na Dhihaak wakasema, "Na ili ulelewe kwa ujuzi Wangu”.

Na hali kadhalika kauli ya Mola, "

{تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا}[2]

Maana yake, "{Ikawa inakwenda mbele ya macho Yetu}".

Maana yake hasa iliyokusudiwa, “Ikawa inakwenda kwa ujuzi Wetu, na hifadhi Yetu”.

Mola aliihifadhi jahazi ya Nabii Nuuh (A.S.) kutokana na hatari ya tufani. Na Nabii Musa (A.S.) alihifadhiwa kutokana na Firauni na watu wake. Mpaka alipofikia umri wa kupewa utume na kumsemesha. Na hiyo khususa kwa Allah ambayo ilikuwa hasa kwa Nabii Musa (A.S.). Na ingelikuwa kweli kauli ya “Na ili ulelewe machoni mwangu,” kama wanavyosema wajinga kuwa anamwona kwa macho Yake, basi Nabii Musa asingelikuwa na fadhila. Kwa sababu Firauni anaona kama anavyoona Nabii Musa. Lakini Mola ametaka, “(تصنع بحفظي)” yaani “(Liundwe chini ya hifadhi au uangalizi Wangu),” mpaka kufikia wakati anaotaka Allah atume ujumbe Wake na hukumu Yake. [1] Surat T`aha aya 39.

[2] Surat al Qamar aya ya 14.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment