Ibadhi.com

27. KUHUSU KAULI YA MOLA: “MOLA WANGU NIONESHE NIKUTAZAME”.

 

869. Jaabir bin Zayd kasema, "Ibn Abbas (R.A.A.) aliulizwa kutokana na kauli ya Allah, "

{رَبِّ أَرِني أَنظُرِ إِلَيْكَ}[1]

 

Maana yake, "{Mola wangu! Nioneshe nikutazame}".

 

Akajibu akasema, "Hiyo ilikuwa kwa ajili ya watu wa Nabii Musa (A.S.) walikataa kumtii isipokuwa kwa kuoneshwa Allah macho kwa macho. Jambo hili lilikuwa muhali kutendeka. Ndipo kukampelekea kumwomba Mola wake dalili za kuwakomesha, na kuwakatiza tamaa zao kwa jambo lisilowezekana kabisa kwa Allah kuonekana na watu”.

 

 

 

870. Umayr bin Ismail bin Ibrahim kasema, "Katusimulia Abu Salih kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.), kutoka kwa Juwaybir, kutoka kwa Dhihaak. Kuhusiana na kauli ya Allah:

 

{سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ}[2]

 

Maana yake, "{Umetakasika! Natubu Kwako}".

 

Hii ni Ni kuhusiana na ombi la (Seyyidina Mussa A.S.) “Nataka nikuone”.

 

{وَأَنَا أَوَّلُ الْمُومِنِينَ}[3]

 

Maana yake, "{Na mimi ni Mwislamu wa kwanza}".

 

Ninasadiki ya kwamba “Hatakuona yeyote”. na Mujaahid kasema kama hivi. Na L-Hasan kasema, " “Hataniona yeyote wala hapaswi yeyote kuniona”.

 

A-Rrabi`i bin Habiyb kasema, " (لن) ni katika herufi za kukata tamaa kwa watu wa Nahau na watu wa lugha, maana yake hawatamuona Duniani wala Akhera”. 

 

Na ama kauli ya Mola, "

 

{فَلَمَّا تَجَلَّى رَبُّهُ لِلْجَبَلِ}[4]

 

Maana yake, "{Basi alipojionyesha Mola wake kwa mlima}".

 

Maana yake hasa iliyokusudiwa, “Zilipodhihiri baadhi ya dalili Zake, jabali halikuweza kuvumilia likaporomoka na kuvurugika, na (Nabii) Musa akaanguka chini amezimia. {Alipozindukana kasema, "{Umetakasika! Nimetubu Kwako} kutokana na ombi langu, {Na mimi ni Mwislamu wa kwanza}”.  Haimpasii kwa kiumbe yoyote yule kuweza kumwona Mola Mtukufu.

 

Mujaahid kasema, "Ikadhihiri hukumu Yake, na kulipasua jabali likawa kama unga”.

 

Ibn Abbas (R.A.A) kasema, " {Muislamu wa kwanza} yaani kuamini kuwa wewe huonekani katika dunia wala Akhera. 

 [1]Surat Al-A`Raaf aya ya 143.

[2] Surat Al-A`Raaf aya ya 143

[3] Surat Al-A`Raaf aya ya 143

[4] Surat Al-A`Raaf aya ya 143.

 

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment