Ibadhi.com

26. KUHUSU KAULI YA MOLA. “ALLAH NI NURU YA MBINGU NA ARDHI”.

 

868. Jaabir bin Zayd kasema, "Ibn Abbas (R.A.A.) aliulizwa kutokana na kauli ya Allah, "

 

{اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ}[1]

 

Maana yake, "{Allah ni nuru ya mbingu na ardhi}".

 

Ibn Abbas (R.A.A.) na L-Hasan, na Qataada, na Amru bin Muhammad, na Abu Muslim L-Makkiy, na Mujaahid wamesema, “Mola ni mweka (haki) sawa mbinguni na ardhini. (Allah) na ndie Mwenye kuwaongoza, na kuwatakasa waliomo mbinguni na ardhini”.

 

Kama vile kauli ya Mola inayosema, " 

 

{مَثَلُ نُورِهِ... }[2]

 

Maana yake, "{Mfano wa Nuru Yake}".

 

Ama kauli ya Mola isemayo, “

 

{...إِلآَّ أَنْ يَّاتِيَهُمُ اللهُ فيِ ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلآَئِكَةُ... }[3]

 

Maana yake, "{Mpaka Allah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika}.

 

Kwa hakika Al-Kulabiyy ametuhadithia kama alivyoipokea kwa Abi Saleh kasema, "Atawaleta kwa amri Yake na hukumu Yake, na atawapambanua baina yao”. Nayo ni kauli ya L-Hasan na Mujaahid" Kama vile kauli ya Mola, "

 

{جَآءَ رَبُّكَ}[4]

 

Maana yake, "{Na kufika (amri ya) Mola wako}. Yaani kwa amri Yake na hukumu Yake.

 

Amesema Ibn Abbas (R.A.A.), na L-Hasan na Abu Salih, na Amru maana ya kauli, "

 

}جَآءَ رَبُّكَ[5]{

 

Maana yake, "{Kufika (amri ya) Mola wako}. Yaani hukumu Yake.

 

Na kadhalika Allah Mtukufu kasema, "

 

{وَلَقَدْ جِئْنَاهُم بِكِتَابٍ... }[6]

 

Maana yake, "{Na hakika tumewaletea Kitabu}. Yaani wamewajia Mitume. Na dalili hiyo inapatikana katika kauli ya Mola Mtukufu katika aya nyingine isemayo, "

 

{هَلْ يَنظُرُونَ إلآَّ أَن تَاتِيَهُمُ الْمَلآَئِكَةُ أَوْ يَاتِيَ أَمْرُ رَبِّكَ}.[7]

 

Maana yake, "{Wanangojea lingine hawa ila Malaika wawafikie, au iwafikie amri ya Mola wako?}.

 

Hushaym aliulizwa kuhusu hayo akasema, "Walikuwa wakisema, "

 

{جَآءَ اَمْرُ رَبِّكَ}[8]

 

Maana yake, "{Na kufika amri ya Mola wako}. Yaani hukumu Yake.

 

Na Allah Mtukufu kasema, "

 

{أَوَلَمْ يَرَوَا اَنَّا نَاتِي الاَرْضَ نَنقُصُهَا مِنَ اَطْرَافِهَا}.[9]

 

Maana yake, "{Jee! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake?}.

 

Na vilevile kasema, "

 

{فَأَتَى اللَّهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ الْقَوَاعِدِ}[10]

 

Maana yake, "{Allah akayasukua majengo[11] yao kwenye misingi}".

 

Na tena kasema, "

 

{فَأَتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا}[12]

 

 Maana yake, "{Lakini Allah aliwaijia kwa mahali wasipopatazamia}".

 [1] Surat An-Nur aya ya 35.

[2] Surat An-Nur aya ya 35.

[3] Surat Al-Baqara aya ya 210.

[4] Surat Al-Fajr aya ya 22.

[5] Surat Al-Fajr aya ya 22.

[6] Surat Al-A`raaf aya ya 52.

[7] Surat An-Nah`l aya ya 33.

[8] Surat Hud aya ya 76 na 101.

[9] Surat R`aad aya ya 41.

[10] Surat An Nah`l aya ya 26.

[11] Akaiharibu miji yao.

[12] Surat Al-Hashri aya ya 2.

 

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment