Ibadhi.com

25. KUHUSU NENO MKONO (اليد).

 

867. Jaabir bin Zayd kasema kwamba, "Ibn Abbas (R.A.A.) aliulizwa kuhusu kauli ya Mola Mtukufu isemayo, "

{وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّهِ مَغْلُولَةٌ}[1]

Maana yake, "{Na Mayahudi wakasema, " {Mkono wa Allah umefungwa}.

Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mayahudi wakasema, "Riziki ya Allah imezuiwa”. Na L-Hasan kasema, "Mola amezuia riziki Yake” (Yaani hivyo ndivyo walivyo kusudia Mayahudi).

Allah Mtukufu kasema, "

{بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ}[2]

Maana yake, "{Bali mikono yake iwazi}".

Ibn Abbas (R.A.A) kasema, "Maana yake, Riziki Yake imeenea kwa viumbe Wake wote”.

{يُنْفِقُ كَيْفَ يَشَآءُ}[3]

Maana yake, "{Hutoa vile apendavyo}".

Ibn Abbas (R.A.A) kasema, "Maana yake, “Huwapa waja awatakao, na kuzuiliwa waja wengine”. Nayo ni kauli ya Mola, "

}يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَّشَاءُ وَيَقْدِرُ{ [4]   

 

Maana yake, "{Allah humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia (amtakaye)}".

Na kwa kauli ya Allah kwa Mtume Wake (S.A.W.), "

{وَلاَ تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً اِلَى عُنُقِكَ وَلاَ تَبْسُطْهَا كُلَّ الْبَسْطِ}[5]

Maana yake, "{Wala usiufanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi}". Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mola amekataza ubakhili na ubadhirifu”.

Dhihaak kasema (katika mkusudio ya aya ifuatayo), "

{بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ}[6]

Maana yake, "{Neema Zake ziko wazi zimeenea na kutanda kotekote}".

{يُنفِقُ كَيْفَ يَشَآءُ}[7]

Maana yake, "{Hutoa vile apendavyo}".[1] Surat Al-Maida aya ya 64.

[2] Surat Al-Maida aya ya 64.

[3] Surat Al-Maida aya ya 64.

[4]Surat Israai aya ya 30

[5] Surat Israai aya ya 29.

[6] Surat Al-Maida aya ya 64.

[7] Surat Al-Maida aya ya 64.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment