Ibadhi.com

24. KAULI YA MOLA “BILA SHAKA TUNGELIMKAMATA KWA MKONO WA KUUME”.

 

866. Ibn Abbas (R.A.A.) kasema kwamba, “(باليمين) maana yake (kwa uwezo)” na L-Hakam bin Uyaynah kasema, "Tafsiri ya maana ya neno (باليمين) ni kwa haki (بالحق)”

 

{لأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ} {ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ}[1]

 

Maana yake, "{Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungalimkata mshipa mkubwa wa moyo}".

 

Dhihaak kasema (باليمين) maana yake, "Kwa uwezo". Na AlKulabiyyi na L-Hasan wakasema, "Maana hiyo hiyo tuliyoitaja nayo ni, "Kwa uwezo".

 [1] Al-Haaqqah aya ya 45 na aya 46.

 

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment