Ibadhi.com

23. KUSUDIO LA NENO MKONO.

 

865. Kauli yake, "

]يَدُ اللَّهِ.. [

Inakusudiwa kwa neno (يَدُ اللَّهِ)  (mkono wa Allah kila linapotajwa ndani ya Quraani) ni kumiliki, na kuwa na uwezo, na wala haikukusudiwa kama vile wanavyomaanisha Wayahudi, kwa sababu kauli yao ni ya ushirikina, na ya Waislamu ni ya kweli. Walivyomaanisha Waislamu ni kinyume na jinsi vile walivyomaanisha Wayahudi. Kwani Wayahudi kusidio lao halikuwa la maana ya kumiliki na kuwa na uwezo, lakini wao wameleta kwa njia ya kufananisha mfano wa mkono wa kawaida.

Na hiyo ni kama kauli ya Allah, "

{تَبَارَكَ الذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ}[1]

Maana yake, “Ametukuka Yule Ambaye Mkononi mwake umo ufalme (wote)”.

Maana yake hasa iliyokusudiwa ni “Wake Mwenyewe (ufalme) wala si wa mwingineo. Wala haimaanishi kushika kama vile anavyoshika mtu mkononi mwake”.

Na hakika ya haya tuyasemayo tuangalie wanavyosema Waarabu, "

نَحْنُ تَحْتَ يَدِ فُلاَنٍ، وَأَمْرُنَا بِيَدِ فُلاَنٍ، وَأَمْرُنَا بِيَدِ اللَّهِ، وَحَوَائِجُنَا بِيَدِ اللَّهِ.

Maana yake, "Sisi tupo chini ya uongozi wa fulani, na jambo letu lipo kwa amri ya fulani, na jambo letu lipo kwa umiliki wa Allah, na haja zetu zipo katika milki ya Allah".

Na Allah kasema, "

{...أَوْ يَعْفُوَ الذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ}[2]

Maana yake, "{Au amesamehe yule ambaye kifungo cha ndoa ki mikononi mwake}".

Na yaliyokusudiwa hapa haya yote yaliyozungumziwa katika Qur-ani, na kilugha ni kumiliki na kudiriki kiuwezo.[1] Surat Al-Mulk aya ya 1.

[2] Surat Al-Baqara aya ya 237.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment