Ibadhi.com

22. KUKAMATA (KUMILIKI).

 

864. Ibn Abbas (R.A.A.) amemuweka katika kundi la washirikina yule atakaesema neno (قبضة) kusudio lake "Si Kumiliki”. Kahukumia kutokana na kauli ya Mola isemayo, "

{سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى عَمَّا يُشْرِكُونَ{[1]

Maana yake, "{Ametakasika, na Ametukuka na hao wanaomshirikisha Naye}".

Na Mola Myukufu kasema, "

{وَاللَّهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ}[2]

Maana yake, “Allah hutoa na huzuia”.

Na pia kasema, "

{ثُمَّ قَبَضْنَاهُ إِلَيْنَا قَبْضًا يَسِيرًا}[3]

Maana yake, “Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo”. Yaani kivuli.

Waarabu husema katika lugha yao, “

 قَبَضَ اللَّهُ فُلاَنًا إِلَيْهِ.

Maana yake, "Allah amemchukua fulani Kwake, maana yake “Amemfisha

 

Na pia wanasema, "

قَبَضَ فُلاَنٌ دَارَهُ وَأَرْضَهُ، يَعْنُونَ بِذَلِكَ: حَازَهُمَا وَمَنَعَهُمَا.

Maana yake, "Fulani ameikamata nyumba yake, na ardhi yake, wanakusudia kusema yu hayi, amevimiliki na amevilinda”.

Na wanasema, "

مَا فُلاَنٌ إِلاَّ فِي قَبْضَتِي مِنْ جِهَةِ الْقُدْرَةِ عَلَيْهِ.

Maana yake, " Fulani yupo chini ya uwezo wangu".

الْخَلْقُ مُتَقَلِّبُونَ فِي قَبْضَةِ اللَّهِ.

Maana yake, Viumbe wapo kwenye uwezo wa Allah katika wayafanyayo.[1] Surat Yunus aya ya 18.

[2]Surat Al-Baqarah aya ya 245

[3] Surat Al-Furqan aya ya 46

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment