Ibadhi.com

20. MAKUSUDIO YA KAULI YA MOLA “KWA WAFANYAO WEMA NI WEMA NA ZAIDI”.

 

860. Jaabir bin Zayd kasema kwamba, "Ibn Abbas (R.A.A.) aliulizwa kuhusu makusudio kauli ya Mola, "

{لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ}[1]

Maana yake, "{Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi} Akasema, "Makusudio yake ni Chumba cha lulu kimoja kina milango minne”.

 

861. Kasema, "Katuhadithia Musa bin Jubayr, kutoka kwa Abdul-Majiyd, na Fudhayl bin `Iyaadh, kutoka kwa Mansur bin Mu`utimar, kutoka kwa L-Hakam bin`Uyaynah, kutoka kwa `Ali bin Abi Taalib (R.A.A.) kasema kama kauli ya Ibn Abbas.[2]

 

862. A-Rrabi`i kasema, "Amepokea Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "

«إِنَّ أَهْلَ الْجَنَّةِ لاَ يَزَالُونَ مُتَعَجِّبِينَ مِمَّا هُمْ فِيهِ حَتَّى يَفْتَحَ اللَّهُ لَهُمُ الْمَزِيدَ، فَإِذَا فُتِحَ لَهُمْ كَانَ لاَ يَأْتِيهِمْ مِنْهُ شَيْءٌ إِلاَّ وَهُوَ أَفْضَلُ مِمَّا فِي جَنَّتِهِمْ»

Maana yake, "{Hakika watu wa Peponi hawataacha kushangaa waliyonayo mpaka Allah awafungulie zaidi. Akiwafungulia itakuwa hakiwajii chochote isipokuwa ni bora kuliko vilivyoko katika Pepo yao}". Allah Mtukufu kasema, "

{وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ}[3]

Maana yake, "{Na kwetu yako ya ziada}".

Jaabir kasema, "Ibn Abbas (R.A.A.) na L-Hasan L-Basry wamesema, "Tamko (الحُسنى بالحسنَةِ) ni jema, kwa jema moja, na tamko (الزيادة) ni kuongezewa mara tisa zilizobakia, Allah Mtukufu kasema, "

{مَن جَآءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا}[4] {مَن جَآءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا}.[5]

Maana yake, "{Atakaekuja na jema, atapata bora kuliko hayo}, {Atakaekuja na jema atalipwa mfano wake mara kumi}".

Na Mujaahid kasema kama alivyosema Ibn Abbas, na L-Hasan, "

     الْحُسْنَى وَالزِّيَادَةُ قَالَ: مَغْفِرَةٌ وَرِضْوَانٌ 

Maana yake ni “Alhusna na Alziada kasema ni, "Msamaha na radhi za Allah”.

Na Sha`abiy kasema, " (الزيادة)" "Ziyada" inamaanisha ni kuingia Peponi”.

Na pia kasema Muhammad bin Ka`ab, "(الزيادة) "Ziyada" inamaanisha, "Allah kuwazidishia karama na thawabu".

Abdu-Rrahman bin Abi Layla kasema neno: “(أَحْسَـنُوا) maana yake, “Wamemuwahidisha Allah”  na neno “(الحسنى) Maana yake, “Pepo”. Na “(الزيادة) inamaanisha, "Allah kuwazidishia fadhila Zake na rehema Zake”.

Na Abu Haazim L-Madaniyy kasema, "(الزيادة) ni: Neema za Allah ambazo alizo waneemesha, amewapa wao, wala hakuwafanyia hesabu katika kuwapa, wala hakuwafanyia wao kama alivyowafanyia wengine, bali amewafunika kwa neema nyingi zisizokuwa na kifani”. [1] Surat Yunus aya ya 26.

[2] Hadithi hii imetajwa katika Hadithi namba 860.

[3] Surat Al Qas`as` aya ya 84.

[4] Surat An Naml aya ya 89.

[5] Surat Al-An-a`am aya ya 160.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment