Ibadhi.com

19. MAANA YA NENO "NADHAR" KATIKA LUGHA YA KIARABU.

 

859. A-Rrabi`i kasema, "Kwa kusadikisha yale tuliyopokea kutoka kwa Masahaba wa Mtume (S.A.W.), na kutoka kwa wafuasi wema, hakika neno (النظر) maana yake ni (الإنتظار) kungojea” Allah kasema, "

{مَا يَنظُرُونَ إِلاَّ صَيْحَةً وَاحِدَةً تَاخُذُهُمْ وَهُمْ يَخَصِّمُونَ}[1]

Maana yake, "{Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wamo kuzozana}". Inayo kusudiwa hapa maana yake ni kungojea wala siyo kwa maana ya kuona kwa macho.

Na pia Kasema, "

{مَا يَنْظُرُ هَؤُلاَءِ اِلاَّ صَيْحَةً وَاحِدَةً مَّا لَهَا مِن فَوَاقٍ}[2]

Maana yake, "{Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda}".

Na pia kasema, " 

{هَلْ يَنظُرُونَ إلآَّ أَن تَاتِيَهُمُ الْمَلآئِكَةُ... }[3]

Maana yake, "{Wanangoja jingine ila wawafikie Malaika}".

Na  ama kusadikisha maana hiyo kwa lugha ya Kiarabu ni kwa kauli ya msemaji, "

)إِنَّمَا أَنْظُرُ إِلَى اللَّهِ ثُمَّ إِلَيْكَ(

Maana yake, “Ninangojea kutoka kwa Allah kisha kutoka kwako”.

Na pia inaweza kuwa kuona ikawa pia bila ya macho. Allah Mtukufu kasema, "

{أَلَمْ تَرَ إِلَى رَبِّكَ كَيْفَ مَدَّ الظِّلَّ}[4]

Maana yake, "{Jee! Huoni vipi jinsi Mola wako anavyokitandaza kivuli}".

Na pia Allah Mtukufu Kasema, "

{أَلَمْ تَرَ إِلَى الذِي حَآجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ... }[5]

Maana yake, "{Jee! Hukumwona yule aliyehojiana na Ibrahim juu ya Mola wake}".

Na tena Allah Mtukufu kasema, "

{أَلَمْ تَرَ إِلَى الذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ... }[6]

Maana yake, "{Jee! Hukuwaona wale waliotoka majumbani kwao}".

Na kadhalika Allah Mtukufu Kasema, "

{أَوَلَمْ يَرَ الاِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ..}[7]

Maana yake, "{Jee! Mwanadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii}".

Na vilevile Allah Mtukufu Kasema, "

{وَلَقَدْ كُنتُمْ تَمَنَّوْنَ الْمَوْتَ مِن قَبْلِ أَن تَلْقَوْهُ، فَقَدْ رَأَيْتُمُوهُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ}[8]

Maana yake, "{Na nyinyi mlikuwa mkitamani mauti kabla hamjakutana nayo. Basi sasa mmekwisha yaona na huku mnayatazama}".

Maneno hayo yote, na mfano wake, yanaonesha wazi si makusudio yake kuonekana kwa macho, na linalokusudiwa ni kuwa na elimu na yakini ya lile jambo. Na ukweli wa haya katika lugha anaweza kusema mtu kwa mfano, “Nimemuona mtu fulani hodari wa kazi au vitendo vyema, na uchamungu, na fahamu na elimu, na nimemuona ana heshima na maarifa, na mambo haya hayaonekani kwa macho lakini yanajulikana, na yanatambulika kwa kudhihirika alama zake zinazojulisha. Na ukimuona mtu mjuzi katika anayotenda, na anayoyawacha, ana hekima katika mambo yake, na anapatia katika ayatendayo, basi utasema nimeona fulani ana akili, na maarifa, na mpangaji, na ikiwa amejiepusha na yaliyoharamishwa utasema namuona mtu huyu mchamungu, ana heshima, na mtu wa kheri.

Amesema Alkumaytu bni Zayd:

رَأَيْتُ اللَّهَ إِذْ أَثْرَى  نِزَارًا ... ... وَأَسْكَنَهُمْ بِمَكَّةَ قَاطِنِيـنَا

Maana yake, "Nilimuona Mwenyezi Mungu[9] walipotajirika Nizaran[10] ..na akawaweka waaishi Makka.

أَيْ مُقِيمِينَ، وَقَالَ أَيْضًا:

رَأَيْتُ اللَّهَ أَهْلَكَ قَوْمَ عَادٍ ... ... ثَمُودَ وَقَوْمَ نُوحٍ أَجْمَعِينَا

Maana yake, "Nimemuoana Allah amewaangamiza watu wa A’ad ……….  Thamuda na watu wa Nuhu wote pamoja"

 

Ametuhadithia Qubaysah, kutoka kwa A’mru bnu Ismaail, kutoka kwa Abi Sinan, kutoka kwa Dhahhaak, kutoka kwa Ali, na Ibn Abbas (R.A.A.) juu ya kauli ya Allah isemayo, "

{كَلآَّ إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ}[11]

Maana yake, "{Sivyo hivyo! Hakika wao kwa Mola wao siku hiyo watazibwa macho wasimuone}".

Ataendelea Allah kuwaziba na kuwanyima rehma Zake na kheri Zake, na wala hatowarehemu. Na kutoka kwa Umayr kutoka kwa Sufyan Aththawriyy utoka Allayth, kutoka kwa Mujahid kauli kama hiyo.[1] Surat Ya-sin aya ya 49.

[2] Surat S`aad aya ya 15

[3] Surat An Nah`l aya ya 33.

[4] Al Furqan aya ya 45.

[5] Surat Al Baqara aya ya 258

[6] Surat Al-Baqara aya ya 243.

[7] Surat Ya-sin aya ya 77

[8] Surat Al-I`mran aya ya 143.

[9] Yaani aliziona rehema na fadhila Zake.

[10] Jina la kikozi au familia.

[11] Surat Al-Mut`affifiin aya ya 15.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment