Ibadhi.com

13. USHIRIKINA UMEFICHIKA KULIKO SAUTI ZA MIGUU YA WADUDU CHUNGU

WADUDU CHUNGU[1] .

830. Kasema, "Na katuambia Muhammad bin Munkadir, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.), kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

«يَأْتِي النَّاسَ زَمَانٌ الشِّرْكُ فِيهِ أَخْفَى مِنْ ذَرَّةٍ سَوْدَاءَ عَلَى صَخْرَةٍ سَوْدَاءَ فِي لَيْلَةٍ ظَلْمَاءَ»

Maana yake, “Utawaijia watu wakati ambao shirki itakuwa imefichikana sana kuliko mdudu chungu mweusi, juu ya jiwe jeusi, katika usiku wa giza jeusi”.

 

831. Jaabir bin Zayd kasema ametuhadithia Anas bin Maalik (R.A.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) kasema, "

«يُوشِكُ الشِّرْكُ أَنْ يَنْتَقِلَ مِنْ رَبْعٍ إِلَى رَبْعٍ، وَمِنْ قَبِيلَةٍ إِلَى قَبِيلَةٍ»

Maana yake, “Inakaribia kuhama shirki kutoka nyumba, mpaka nyumba nyingine, na kutoka kabila, mpaka kabila lingine”.  Ikaulizwa, “Ewe Mtume wa Allah ni shirki gani hiyo?” Akajibu akasema, "

«قَوْمٌ يَأْتُونَ مِنْ بَعْدِكُمْ يَحُدُّونَ اللَّهَ حَدًّا بِالصِّفَةِ».

Maana yake, “Watakuja watu baada yenu, watamwekea Allah vizingiti (au mpaka), kwa kumsifu (kwao)”.

 

832. Kasema, "Na ametuhadithia A`amash, kutoka kwa Abi Waa-il, kutoka kwa Ibn Mas`uud (R.A.A.) kasema, "Nilimwuliza Mtume (S.A.W.) dhambi gani iliyo kubwa zaidi?” Akajibu akasema, "

«أَنْ تَجْعَلَ لِلَّهِ نِدًّا وَهُوَ خَلَقَكَ، وَاللَّهُ الْعَدْلُ».

Maana yake, “Kukifanya kitu kingine kuwa sawa na Allah. Naye kakuumba. Na Allah ni Muadilifu”.

 

833. Kasema na ametuambia Sufyaan bin Uyayna, kutoka kwa Mujaahid bin Sa`id, kutoka kwa Sha`abiy, kutoka kwa Jaabir bin Abdallah kasema, "Wayahudi walimwambia Mtume (S.A.W.), “Ewe Muhammad! Rafiki zako wameshindwa leo hii”. Akajibu akasema, "

«بِأَيِّ شَيْءٍ»؟

Maana yake, “Kwa kitu gani?” Wakasema, "Wayahudi waliwauliza, “Jee, Mtume wenu anafahamu idadi ya walinzi wa Motoni?” Wakajibu wakasema, "Hatujui mpaka tumwulize Mtume wetu”. Mtume (S.A.W.) akasema, " 

«نِعْمَ مَا فَعَلُوا، قَوْمٌ يُسْأَلُونَ عَمَّا لاَ يَدْرُونَ فَقَالُوا لاَ نَدْرِي حَتَّى نَسْأَلَ نَبِيَّنَا»

Maana yake, “Ni jambo jema walilofanya watu kuja kuulizwa wasiyojua, wakajibu hatujui, mpaka tumwulize Mtume wetu”. Kisha (Mtume) (S.A.W.) akasema, "

«يَا أَعْدَاءَ اللَّهِ وَلَكِنْ تَسْأَلُونَ نَبِيَّكُمْ أَنْ يُرِيَكُمُ اللَّهَ جَهْرَةً»

Maana yake, “Enyi maadui wa Mwenyezi Mungu! Lakini nyinyi mlimwomba Mtume wenu awaonesheni Mola wazi wazi”. Akawaambia Mtume wa Allah walipomtaka  awaonyeshe Allah, kuwa, "Hakika Allah haonekani wazi wazi”.

 

834. A-Rrabi`i kasema, "Tuliarifiwa na Abaan bin Ayyaash, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) aliwatokea watu waliokuwa wamekaa akasema, "

«مَا أَجْلَسَكُمْ»؟

Maana yake, “Nini kilichowakalisheni?” Wakasema, "Tunamfikiria Allah”. Mtume (S.A.W.) akasema, "

«لاَ تَتَفَكَّرُوا فِي اللَّهِ فَإِنَّهُ لاَ مِثْلَ لَهُ وَلاَ شَبِيهَ وَلاَ نَظِيرَ وَلاَ تَضْرِبُوا لِلَّهِ الأَمْثَالَ، وَلاَ تَصِفُوهُ بِالزَّوَالِ، فَإِنَّهُ بِكُلِّ مَكَانٍ، وَتَفَكَّرُوا فِي خَلْقِهِ، وَلأُخْبِرَنَّكُمْ بِبَعْضِ خَلْقِهِ: إِنَّ مَلَكًا مِنَ الْمَلاَئِكَةِ لَهُ جَنَاحٌ بِالشَّرْقِ وَجَنَاحٌ بِالْغَرْبِ، وَقَدْ خَرَقَتْ رِجْلاَهُ الأَرَضِينَ  السُّفْلَى، وَرَأْسُهُ فِي السَّمَاءِ السَّابِعَةِ».

Maana yake, “Msimfikirie Allah. Kwa hakika Yeye hafanani na chochote, na hashabihiani na chochote, na wala msipigie mifano, na wala msimsifie kwa kuhamahama (kutoka pahala fulani na kwenda mahali pengine). Kwa hakika Yeye yupo kila sehemu. Na fikirieni katika viumbe Wake.  Na nitakwambieni baadhi ya viumbe Vyake, kuna mmoja wa Malaika katika Malaika (Wake) ana ubawa upande wa Mashariki, na ubawa mwingine upande wa Magharibi, miguu yake miwili imepasua ardhi ya chini, na kichwa chake kiko mbingu ya saba”.[1] Sisimizi.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment