Ibadhi.com

11. AMENIELIMISHA MAARIFA YA MAMBO YALIOFICHIKA.

 

 

 

826. A-Rrabi`i bin Habiyb, kutoka kwa Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Alikuja Bedui mmoja kwa Mtume (S.A.W.) akasema, "Nifundishe maarifa ya kuyajua yaliofichika na mageni (ya ajabu) akasema, "

 

«وَمَا صَنَعْتَ فِي رَأْسِ الْعِلْمِ حَتَّى تَسْأَلَ عَنْ غَرَائِبِهِ»؟

 

Maana yake, “Umefanya nini katika kichwa cha maarifa, na ujuzi, hata ukayauliza yasiyojulikana, na yaliyo mageni?” Akasema (Bedui), “Nini kichwa cha maarifa?” Akasema, "

 

«مَعْرِفَةُ اللَّهِ حَقَّ مَعْرِفَتِهِ»

 

Maana yake, “Kumjua Allah kama inavyotakikana”.

 

Akasema, "Namna gani kumjua Allah vilivyo?” Akasema (Mtume (S.A.W.), "

 

«أَنْ تَعْرِفَهُ بِلاَ مِثْلٍ وَلاَ نِدٍّ، وَاحِدًا، أَحَدًا، ظَاهِرًا، بَاطِنًا، أَوَّلاً، آخِرًا، لاَ كُفْؤَ لَهُ، فَذَلِكَ مَعْرِفَةُ اللَّهِ حَقَّ مَعْرِفَتِهِ».

 

Maana yake, “Umjue bila mfano, wala mpinzani, Mmoja Aliye pekee bila ya mshirika, Anayajua yaliyo dhahiri (yenye kuonekana), na ya ndani (yasiyoonekana), wa Mwanzo, na wa Mwisho, hana aliyefanana Nae. Na huko ndiko kumjua Allah kwa yakini, na hivi ndivyo kumjua Mola vilivyo”. 

 

 

 

Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«إِنَّ اللَّهَ لاَ يُعْرَفُ بِالأَمْثَالِ وَلاَ بِالأَشْبَاهِ، وَإِنَّمَا يُعْرَفُ بِالدَّلاَئِلِ وَالأَعْلاَمِ الشَّاهِدَةِ عَلَى رُبُوبِيَّتِهِ، النَّافِيَةِ عَنْهُ آثَارَ صَنْعَتِهِ».

 

Maana yake, “Hakika Allah hajulikani kwa njia ya mfano, wala kumshabihisha[1]. Walakini kujulikana Kwake ni kwa dalili, na kwa ulimwengu unaoonekana juu ya ubwana na ulezi wake, na kutomfananiza na alivyoviumba ”.

 [1] Kumfananisha.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment