Ibadhi.com

10. SUNNA KATIKA KUMUADHIMISHA MOLA MTUKUFU.

 

 Yaliyo hadithiwa kutoka kwa Mtume (S.A.W.), na Masahaba Zake, na wafuasi wa Masahaba waliokuwa wema (Taabi`iyna).

 821. Jaabir kasema kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.), “Mtu mmoja wa kabila la Bani Amiir bin Rabia aliyeitwa Arbad alikuja mbele ya Mjumbe wa Allah (S.A.W.) akasema, "Ewe Muhammad (hebu) niambie huyo Mola wako anatokana na dhahabu au fedha, au shaba au chuma? Na huku Mtume (S.A.W.) akisema,"

 «سُبْحَانَ اللَّهِ!»

 Maana yake, “Ametakasika Mola,” mara ikapiga radi ya nguvu na umeme mzito, na ukachomoka mshale wa mwanga wa moto utakao radini ukampiga (yule mtu) kichwani mwake akaanguka (chini) ilhali amefariki dunia. Na Allah Mtukufu kasema, "  

 {وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَنْ يَّشَآءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللَّهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ}[1]

 Maana yake, {Naye hupeleka mapigo ya radi na kumpiga nayo amtakaye. Nao wanabishana juu ya Allah. Na Yeye ni Mwenye adhabu kali!}.

 

822. Jaabir bin Zayd kasema kutoka kwa Sa`id bin Jubair (R.A.A), kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Wayahudi walimuuliza Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kuhusu sifa za Allah, akanyamaza kidogo akitarajia kuwateremkia adhabu ya Mola. Kisha Jibril (A.S.) akateremka na Surat Al-Ikhlaas, " 

 {بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ...} إِلَى آخِرِهَا.

 Maana yake, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu wa Rehema Mwenye Kurehemu. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee…….Mpaka mwisho wa Sura".

 

823. Na Mtume wa Mola (S.A.W.) kasema, "

 «تَفَكَّرُوا فِي الْخَلْقِ وَلاَ تَتَفَكَّرُوا فِي الْخَالِقِ، فَإِنَّهُ لاَ يُدْرَكُ إِلاَّ بِتَصْدِيقِهِ».

 Maana yake, “Fikirieni juu ya viumbe, na wala msifikirie juu ya Muumbaji. Kwa hakika (macho) hayamfikilii isipokuwa kwa kumwamini vilivyo”.

 

824. A-Rrabi`i kasema, "Ametuambia Bishr, kutoka kwa Ismail bin `Ulayya, kutoka kwa Daud bin Abi `Uqayl, kutoka kwa Abi Hind, kutoka kwa Sha`abiyyi, kutoka kwa Masrouq kasema, "Nilikuwa kwa Aisha (R.A.A.H.) akasema, "

 ثَلاَثَةٌ مَنْ تَكَلَّمَ بِوَاحِدَةٍ مِنْهُنَّ فَقَدْ أَعْظَمَ عَلَى اللَّهِ الْفِرْيَةَ: مَنْ زَعَمَ أَنَّ مُحَمَّدًا رَأَى رَبَّهُ فَقَدْ أَعْظَمَ عَلَى اللَّهِ الْفِرْيَةَ.

 Maana yake, “Matatu (katika haya) atakaelizungumza moja kati ya hayo atakuwa amemsingizia uwongo mkubwa Allah. Atakaesema kwamba Muhammad alimuona Mola wake atakuwa kamzulia uwongo mkubwa Allah”. Akasema, "Nilikuwa nimeegemea nikaa kitako nikasema, "Ewe mama wa Waislamu! Niangalie wala usifanye haraka jee, Allah hakusema:

 {وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً اُخْرَى} -- {وَلَقَدْ رَآهُ بِالاُفُقِ الْمُبِينِ}

 Maana yake, “{Na akamwona mara nyingine [2]} -- {Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi[3]} Aisha (R.A.A.H) akasema, "Mimi ni wa mwanzo katika umma huu niliyemwuuliza Mtume (S.A.W.) kuhusu haya akasema, "

 «ذَلِكَ جِبْرِيلُ عَلَيْهِ السَّلاَمُ وَلَمْ أَرَهُ فِي صُورَتِهِ التِي خُلِقَ عَلَيْهَا إِلاَّ مَرَّتَيْنِ قَدْ هَبَطَ مِنَ السَّمَاءِ فَسَدَّ جِسْمُهُ مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ»، أَلَمْ تَسْمَعْ لِقَوْلِهِ تَعَالَى:

Maana yake, “Huyo alikuwa Jibril (A.S.), wala sijamwona katika sura yake aliyoumbiwa isipokuwa mara mbili, nilimwona wakati alipokuwa akiteremka kutoka mbinguni, kiwiliwili chake kiliziba uwazi ulioko kati ya mbingu na ardhini. Jee, hukusikia kauli ya Allah Mtukufu inayosema, "

{لاَّ تُدْرِكُهُ الاَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الاَبْصَارَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ}؟  [4]

 Maana yake, “Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari”. Masrouq kasema, "Tafsisri ya aya hii ni dalili ya wazi aliyosimulia Bibi Aisha (R.A.A.) kutoka kwa Mtume (S.A.W.) inayosema, "

 {مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَى} [5]  {لَقَدْ رَأَى مِنَ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَى} [6]

 Maana yake, “Moyo haukusema uwongo uliyoyaona. Kwa yakini (Mtume Muhammad) aliona mambo makubwa kabisa katika alama, (Qudra) za Mola wake”. Tena akairudia kuitaja Hadithi ya Ulayyah akasema, "Kasema Aisha (R.A.A.H.), "

 وَمَنْ زَعَمَ أَنَّ مُحَمَّدًا صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يُبَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ فَقَدْ أَعْظَمَ عَلَى اللَّهِ الْفِرْيَةَ، لأَنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَقُولُ:

 Maana yake, “Na atakaedai ya kwamba Muhammad (S.A.W.) hakufikisha ujumbe ulioteremshwa kutoka kwa Mola wake amemsingizia uwongo mkubwa Allah. Kwani Allah anasema, "

  }يَـأَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ إِنَّ اللَّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ{ [7]

 Maana yake, "{Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Allah atakulinda na watu, na Allah haongoi watu makafiri}". Na atakaedai kwamba Muhammad (S.A.W.) anajua yatakayotokea kesho atakuwa amemsingizia uwongo mkubwa Allah. Kwa sababu Allah anasema, "

 }قُل لاَّ يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاواتِ والأَرْضِ الْغَيْبَ إِلاَّ اللَّهُ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ{[8]

 Maana yake, "{Sema: “Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipokuwa Allah. Wala wao hawajui lini watafufuliwa}.

 

825. Ametuambia Abu Rabiy`a Zayd bin `Auf L-`Aamiry L-Basary kasema, "Katuambia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit L-Bannaniy, kutoka kwa Abi `Uthmaan Nnahdiy kwamba Abu Musa L-Ash`ary kasema, "Tulikuwa pamoja na Mtume wa Mola (S.A.W.) katika safari, tulipokuwa tunaukaribia mji wa Madina watu wakapiga Takbiyr, na wakapaza sauti zao kisha Mtume (S.A.W.) akasema, "

 «يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّكُمْ لاَ تَدْعُونَ أَصَمَّ وَلاَ غَائِبًا إِنَّ الذِي تَدْعُونَهُ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ أَعْنَاقِ رِكَابِكُمْ»، ثُمَّ قَالَ:

 Maana yake, “Enyi watu! Kwa hakika nyinyi hamumuombi kiziwi wala asiye kuwepo. Hakika ambae mnamuomba yupo kati yenu, na baina ya shingo za vipando vyenu”.  Kisha akasema, "

 «يَا أَبَا مُوسَى هَلْ أَدُلُّكَ عَلَى كَنْزٍ مِنْ كُنُوزِ الْجَنَّةِ؟»

 Maana yake, “Ewe Aba Musa! Jee, nikwambie kuhusu khazina mojawapo ya khazina za Peponi? Kasema, "Nikasema, "Ni nini hiyo ewe Mtume wa Allah?, Akasema, "La Hawla wala Quwwata illa bi-Llaahi”.

 

Kasema Jaabir, "Maana ya kauli ya Mtume (S.A.W.) kwetu sisi, "

 

«إِنَّ الذِي تَدْعُونَهُ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ أَعْنَاقِ رِكَابِكُمْ»

 

Maana yake, “Hakika ambae mnamuomba yupo kati yenu, na baina ya shingo za vipando vyenu”.  Hayo ni kwa maana ya maneno ya Mola Mtukufu, "

 

{مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَى ثَلاَثَةٍ اِلاَّ هُوَ رَابِعُهُمْ وَلاَ خَمْسَةٍ اِلاَّ هُوَ سَادِسُهُمْ وَلآ أَدْنَى مِن ذَالِكَ وَلآ أَكْثَرَ إِلاَّ هُوَ مَعَهُمُ, أَيْنَ مَا كَانُوا}[9]

 

Maana yake, {Haupatikani mnong`ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wa nne wao, wala watano ila Yeye huwa ni wa sita wao, wala wa wachache kuliko hao wala zaidi ila Yeye huwa pamoja nao popote walipo}. Na Akasema, "

 

}وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ {[10]

 

Maana yake, {Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni (mwake)}. [11]

 [1] Surat Ar-Raa`d aya ya 13.

[2] Surat AnNajm aya ya 13.

[3] Surat At-Takwiir aya ya 23.

[4] Surat An-a`am aya ya 103.

[5] Surat An-Najm aya ya 11.

[6] Surat An-Najm aya ya 18.

[7] Surat Al-Maida aya ya 67.

[8] Surat An-Naml aya ya 65.

[9] Surat al Mujadalah aya ya 7.

[10]  Surat Qaaf aya ya 16

[11] Mifano ya masafa na vipimo huongewa na viumbe wenye kuumbwa, kwani tukiangalia kwa makini, tutaona kiumbe akikaribia sehemu fulani huwa mbali na nyingine. Na akiwa katika mahali Fulani, huwa hayupo sehemu nyingine, kwa sababu masafa yanahitajia kuondoka na kusafiri safiri mara hapa, na mara kule. Lakini Allah Mtukufu yuko mbali na upungufu huo.

 

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment