Ibadhi.com

9. ADHABU YA KABURI, MASHAHIDI, KUWAPENDA MAQURAISHI, NA UTIIFU WA VIONGOZI.

 

812. Jaabir bin Zayd kasema, "Aliulizwa Ibn Abbas (R.A.A.) kuhusu adhabu ya kaburini, akasema, "Mtume wa Allah kasema, "

«إنَّ لِلْقَبْرِ مَلَكَيْنِ يُقَالُ لَهُمَا: مُنْكَرٌ وَنكِيرٌ، يَأْتِيَانِ كُلَّ إِنْسَانٍ فِي قَبْرِهِ بَعْدَ مَوْتِهِ، يَمْتَحِنَانِهِ، ثُمَّ يُحَاكِمَانِهِ».

 Maana yake, “Hakika katika kaburi kuna Malaika wawili wanaoitwa Munkar na Nakiyr, humjia kila mtu kaburini mwake, baada ya kifo chake, humfanyia mtihani (wa maswali), na kumhukumu mtu huyo”.

 

813. Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

 «لَوْ نَجَا مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ أَحَدٌ لَنَجَا مِنْهُ سَعْدُ بْنُ مُعَاذٍ، وَلَقَدْ ضَغَطَهُ الْقَبْرُ ضَغْطَةً اخْتَلَفَتْ فِيهِ أَضْلاَعُهُ».

 Maana yake, “Lau angeliokoka mtu na adhabu ya kaburi basi angeliokoka Sa`ad bin Mu`adh (R.A.A). Kwani alibanwa na kaburi mpaka mbavu zake (za kuliani na kushotoni) zikapishana”.

 

814. Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

 «الشَّهِيدُ يُغْفَرُ لَهُ عِنْدَ أَوَّلِ قَطْرَةٍ تَقْطُرُ مِنْ دَمِهِ، وَيُجَارُ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ».

 Maana yake, “Shahidi (aliyekufa katika vita baina ya Waislamu na makafiri) husamehewa madhambi yake wakati wa kudondoka tone la kwanza la damu yake, na huepushwa na adhabu ya kaburi”.

 

815. Mtume (S.A.W.) kasema, "

 «مَنْ مَاتَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ أُجِيرَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ».

 Maana yake, “(Mwislamu) atakaekufa siku ya Ijumaa (au usiku wa kuamkia Ijumaa) ataepushwa na adhabu ya kaburi”.

 

816. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 «إِنْ لَمْ يَكُنِ الشُّهَدَاءُ مِنْ أُمَّتِي إِلاَّ مَنْ قُتِلَ بِالسَّيْفِ فَهُمْ إِذَنْ قَلِيلٌ» ثُمَّ قَالَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْقَتِيلُ شَهِيدٌ...»

 Maana yake, “Na lau ingalikuwa hawawi mashahidi katika umma wangu ila aliyekufa kwa kupigwa upanga basi wangelikuwa wachache”. Kisha akasema, "Aliyeuliwa ni shahidi”. [1].

 

817. Jaabir bin Zayd kasema, "Aliulizwa Ibn Abbas (R.A.A.) kuhusu kufadhiliwa Ma-Qurayshi akajibu akasema, "Mtume wa Mola (S.A.W.) kasema, "

 «اللَّهُمَّ كَمَا أَذَقْتَ أَوَّلَ قُرَيْشٍ نَكَالاً، فَأَذِقْ آخِرَهُمْ نَوَالاً».

  Maana yake, “Ewe Allah! Kama ulivyowaonjesha adhabu (mashaka) Maquraishi wa mwanzo, basi wa mwisho wao wafadhili, waonee huruma (wape kheri)”.

 

818. Na Mtume wa Mola (S.A.W.) kasema, "

 «لَنْ يَزَالَ هَذَا الأَمْرُ فِي قُرَيْشٍ مَا لَمْ يُحْدِثُوا أَحْدَاثًا، ثُمَّ يُزِيحُهُ اللَّهُ عَنْهُمْ وَيَلْحَاهُمْ كَمَا يُلْحَى هَذَا الْقَضِيبُ» لِقَضِيبٍ كَانَ فِي يَدِهِ.

 Maana yake, “Halitaondolewa hili jambo kwa Ma-Quraishi ikiwa hawatazua bidaa, Halafu Allah ataliondoa kutoka kwao, na atawachuna kama ilivyochunwa fimbo hii”. (Fimbo ambayo alikuwa nayo mkononi).

 

819. Na Mtume wa Mola (S.A.W.) kasema, "

 «إِنْ أُمِّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حَبَشِيٌّ مَجْذُوعُ الأَنْفِ، فَاسْمَعُوا وَأطِيعُوا مَا أَقَامَ فِيكُمْ كِتَابَ اللَّهِ».

 Maana yake, “Mkipewa kiongozi juu yenu mtumwa wa Kihabeshi amekatwa pua, msikilizeni na mtiini iwapo atawahukumuni kwa (sheria) za Kitabu cha Allah”.

 

820. Na Mtume wa Mola (S.A.W.) kasema, "

 «يَا فَاطِمَةُ بِنْتَ مُحَمَّدٍ، وَيَا صَفِيَّةُ عَمَّةَ مُحَمَّدٍ، اِشْتَرِيَا أَنْفُسَكُمَا مِنَ اللَّهِ، فَإِنِّي لاَ أَمْلِكُ لَكُمَا مِنَ اللَّهِ شَيْئًا»

 Maana yake, “Ewe Fatima binti Muhammad (S.A.W.)! Na ewe Safiyya shangazi wa Muhammad (S.A.W.) Jinunulieni nafsi zenu kwa Allah. Kwa hakika mimi similiki chochote kwa ajili yenu kwa Allah”.[2]

 [1] Hadithi hii imetajwa katika Hadithi namba 450.

[2] Ikiwa maelezo haya kayatoa Mtume (S.A.W.) kwa binti yake, na shangazi yake. Basi itakuwaje kwa mwengineo ambao si kama hawa ambaye anataka asamehewe madhambi yake na huku kabobea kwenye madhambi na hakutubu.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment