Ibadhi.com

6. KULINGANIA KATIKA UISLAMU NA KUKATAZWA VITA.

 

 

792. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd kasema, "Nimepata khabari ya kwamba Mtume (S.A.W.) alimtuma Ali kuliongoza jeshi dogo akasema, "

 

«يَا عَلِيُّ، لاَ تُقَاتِلِ الْقَوْمَ حَتَّى تَدْعُوَهُمْ وَتُنْذِرَهُمْ، فَبِذَلِكَ أُمِرْتُ».

 

Maana yake, “Ewe Ali! Usipigane (vita) na watu mpaka uwaite katika uisilamu, na uwaonye (uwalinganie) kwa haya ndivyo (hivyo) nilivyoamrishwa”. Akasema nilishtuka kuletewa kundi la mateka kutoka katika mtaa mmoja wa mitaa ya Waarabu, wakasema, "Ewe Mjumbe wa Mola! Hapana aliyetulingania wala aliyetufikishia” akasema, "Allah,” wakasema, "Allah, akasema, "

 

«خَلُّوا سَبِيلَهُمْ»

 

Maana yake,  “Wafunguweni na waacheni waende zao,” halafu akasema, "

 

«حَتَّى تَصِلَ إِلَيْهِمْ دَعْوَتِي فَإِنَّ دَعْوَتِي تَامَّةٌ لاَ تَنْقَطِعُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ»

 

Maana yake, “Mpaka uwafikie wito wangu, kwani wito wangu umekamilika, haukatiki mpaka siku ya Kiyama”. Baadaye Mtume (S.A.W.) alisoma aya hii:

 

{وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَذَا القُرْءَانُ لأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ...} إِلَى آخِرِ الآيَةِ.[1]

 

Maana yake, {Na nimefunuliwa Qur-ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayomfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Allah wapo miungu wengine?” Sema, “Mimi sishuhudii hayo”. Sema, “Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnaowashirikisha}.

 

 

 

793. Kasema, "Na akasema Ibn Umar (R.A.A.) na L-Hasan L-Basry (R.A.A.) wakasema, "Kwamba wito wa Mtume (S.A.W.) umekwishatimia katika uhai wake, na umekatika baada ya mauti yake. Hapana wito leo.  

 

A-Rrabi`i kasema, "Abu Ubayda kasema, "Wito haujakatika mpaka siku ya Kiyama, isipokuwa atakaekuja kwako ghafla akakutaka upigane naye, (hapo) itakubidi upigane naye kwa ajili ya kuilinda nafsi yako bila ya wito”.

 [1] Surat An-A`am aya ya 19.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment