Ibadhi.com

5. MAKATAZO YA KUUA WATOTO, NA WANAWAKE.

 

791. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas, kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«إِيَّاكُمْ وَقَتْلَ ذَرَارِي الْمُشْرِكِينَ وَنِسَائِهِمْ إِلاَّ مَنْ قَاتَلَ مِنْهُمْ فَإِنَّهَا تُقْتَلُ».

 

Maana yake, “Ole wenu kuuwa vizazi vya washirikina, na wake zao, isipokuwa yule mwanamke atakayeingia vitani kupigana (na nyinyi), huyo huuwawa”.

Kasema kwamba Mjumbe wa Allah (S.A.W.) aliwazingira, na kuwazunguka watu wa ngomeni (Khaybar), na alikuwepo mwanamke mmoja kaingia vitani kupigana, yeye alikuwa akiuonesha utupu (uchi) wake na kumwelekea Mtume (S.A.W.),  na huku anapigana. Mjumbe wa Allah (S.A.W.) aliwaamrisha wapigaji mishale wampige mshale, Sa`ad bin Abi Waqaas (R.A.A.) akampiga mshale bila kumkosea akaporomoka kutoka ngomeni naye maiti.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment