Ibadhi.com

4. KUKATAZA MABAYA.

 

789. A-Rrabi`i kasema, "Abu Ubayda kasema, "Nimepata habari itokayo kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.) ya kwamba kasema, "

 

«لاَ يَمْنَعَنَّ أَحَدَكُمْ مَخَافَةُ النَّاسِ أَنْ يَتَكَلَّمَ بِالْحَقِّ إِذَا شَاهَدَهُ، وَيُنْكِرَ الْبَاطِلَ إِذَا قَدِرَ عَلَيْهِ».

 

Maana yake, “Hapana kizuizi cha kumzuia mmoja wenu asiseme haki akiiona, na kukataza mabaya ikiwa ana uwezo”.

 

790. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«قُلِ الْحَقَّ وَلَوْ كَانَ مُرًّا، وَلاَ تُشْرِكْ بِاللَّهِ شَيْئًا وَإِنْ عُذِّبْتَ أَوْ أُحْرِقْتَ »

 

Maana yake, “Sema haki japokuwa ni chungu, wala usimshirikishe Allah na kitu chochote kile, japokuwa kutakupelekea kuteswa (kuadhibiwa), au kuunguzwa moto”.

 

A-Rrabi`i kasema, kutoka kwa Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, maana ya hayo ni, "Kumshirikisha kwa moyo, ama kwa ulimi ameruhusu, na kujuzisha Allah, kwa aliyelazimishwa kwa nguvu bila hiari.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment