Ibadhi.com

3. HOJA YA KULAZIMIKA KUSALIWA MAITI WA KIBLA KIMOJA; NA KUSALI NYUMA YA MWEMA NA ASIYE MWEMA.

 

776. A-Rrabi`i bin Habiyb Mola amrehemu kasema kwamba, "Nilimsikia Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A,) kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«الصَّلاَةُ جَائِزَةٌ خَلْفَ كُلِّ بَارٍّ وَفَاجِرٍ، وَصَلُّوا عَلَى كُلِّ بَارٍّ وَفَاجِرٍ».

 

Maana yake, “Sala inajuzu kusaliwa nyuma ya kila aliyemwema, na muovu, na wasalieni kila aliye mwema na muovu”.[1]

 

777. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«الصَّلاَةُ عَلَى مَوْتَى أَهْلِ الْقِبْلَةِ الْمُقِرِّينَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَاجِبَةٌ فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ».

 

Maana yake, “Sala kwa ajili ya maiti wa kibla kimoja (Waislamu) waliomkubali Allah (Mmoja), na Mtume Wake (S.A.W.), na siku ya Mwisho, ni wajibu kusaliwa, na atakaeiacha amekufuru”.

 

778. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«رَحِمَ اللَّهُ مَنْ سَكَتَ فَسَلِمَ أَوْ قَالَ فَغَنِمَ».

 

Maana yake, “Allah amemrehemu aliyenyamaza, na akasalimika, au akasema akafanikiwa”.

 

779. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«لاَ تَكُنْ طَعَّانًا وَلاَ لَعَّانًا، وَلاَ تَقُلْ فِي الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَنْ بِهِ اللَّهُ».

 

Maana yake, “Usiwe mtukanaji, wala mlaanaji[2], na wala usiseme katika dini asiyoyatolea idhini Allah”.

 

780. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«سَتَكُونُ مِنْ بَعْدِي أَئِمَّةٌ لاَ يَسْتَنُّونَ بِسُنَّتِي وَلاَ يَهْتَدُونَ بِهُدَايَ»، فَقَالُوا: كَيْفَ الْمَخْرَجُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ فَقَالَ: «أَطِيعُوهُمْ مَا لَمْ يَمْنَعُوكُمُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسَ»

 

Maana yake, “Baada yangu watakuwepo viongozi (ambao) hawatafuata Sunna yangu, wala kuongoka kwa uwongofu wangu”. Wakasema, "Vipi tufanye katika hii, ewe Mtume wa Mola?” Akajibu, “Muwatii ikiwa hawatawazuia (kuzisali) Sala tano”.

 

Umar (R.A.A.) kasema, "Mtiini Imamu japokuwa atakupiga, au kukunyima (jambo), au kukudhulumu, kwani Mtume (S.A.W.) ameamuru kumtii Amiri (Kiongozi) hata kama hahukumu kisheria, na kumsalia atakapokufa, basi vipi kwa wengine watu wa kibla kimoja? Ambao wanamkubali Allah, na Malaika Wake, na vitabu Vyake, na Mitume Wake, na siku ya Mwisho. Na atakaesema yasiyo kuwa haya kakufuru kufuru isiyo kuwa ya kushiriki”.    

 

781. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«لِيَؤُمَّكُمْ خِيَارُكُمْ فَإِنَّهُمْ وَفْدُكُمْ إِلَى رَبِّكُمْ».

 

Maana yake, “Awasalisheni mbora wenu, kwa hakika wao ni wawakilishi wenu kwa Mola wenu”.

 

782. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«لاَ صَلاَةَ لإِمَامٍ أَمَّ بِقَوْمٍ وَهُمْ لَهُ كَارِهُونَ».

 

Maana yake, “Hapana Sala kwa Imamu anayesalisha watu nao hawamtaki”.

 

783. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«لِيَلِنِي فِي الصَّفِّ الأَوَّلِ أُوْلُو النُّهَى مِنْكُمْ ثُمَّ الذِينَ يَلُونَهُمْ ثُمَّ الذِينَ يَلُونَهُمْ».

 

Maana yake, “Wanikaribie katika mstari wa kwanza walio makini, na busara miongoni mwenu. Kisha ambao wanafuatia. Kisha ambao wanafuatia”.

 

784. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«تَخَيَّرُوا لإِمَامَتِكُمْ، وَتَخَيَّرُوا لِنُطَفِكُمْ».

 

Maana yake, “Mchaguweni Imamu wenu, na mchague kwa ajili ya kila tone lenu la uzazi”. (Yaani mchague mbora katika nyinyi kuwa imamu wenu, na muwachagueni wanawake walio bora kuwa wake zenu wenye tabia njema).

 

785. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«لَعَنَ اللَّهُ الْمُسَلَّطَ عَلَى أُمَّتِي بِالْجَبَرُوتِ وَالْمُسْتَأْثِرَ بِفَيْئِهَا».

 

Maana yake, “Mola anamlaani anayeutawala umma wangu kwa ujabari[3], na mwenye kufanya upendeleo kwa walio karibu nae, au chini yake”.

 

786. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

 

«أَيُّمَا أَمِيرٍ ظَالِمٍ فَهُوَ خَلِيعٌ، وَأَيُّمَا أَمِيرٍ ظَالِمٍ فَلاَ إِمَارَةَ لَهُ، فَلْيَسْتَخِرِ اللَّهَ مَنْ بِحَضْرَتِهِ مِنَ الْمُسْلِمِينَ، أَوْ لِيُوَلُّوا عَلَيْهِمْ أَفْضَلَ فُضَلاَئِهِمْ فِي أَنْفُسِهِمْ».

 

Maana yake, “Amiri (Kiongozi) yeyote yule dhalimu ametolewa (yaani anatabirika kaenguliwa), na Amiri yeyote yule dhalimu hapewi uongozi, watu wamuombe Allah Mtukufu ushauri katika kuchagua kati ya wale walioko katika Waisilamu, au wamtawalishe aliyekuwa mbora kwao walieridhika naye”.

 

787. Na Umar bin Khattaab (R.A.A.) kasema, "Jambo hili haliwezi kukaa sawa isipokuwa kwa mwenye sifa tano, na ikipungua moja tu haiwezekani mambo manne ila matano. Kukusanywa mali kutokana na chanzo cha halali. Kukinai na kutoitamani baada ya kukusanywa, na kuwakabidhi wenye kustahiki baada ya kukusanywa. Upole usio na udhaifu, Ukali usio na udikteta.

 

788. Na Ali bin Abi Taalib (R.A.A.) alipowatuma wajumbe wake kwenda kwa Ma`awiyah bin Abi Sufyaan kasema, "Salini juu ya vipando vyenu vya usafiri. Na jalieni Sala yenu pamoja nao ni sala ya nyongeza (sunna), kwani Allah hakubali ila kwa wamchao Mola”. Na alikuwa L-Hasani L-Basry (R.A.A.) na Said bin Jubayr (R.A.A.) walikuwa wakisali Ijumaa majumbani mwao. na baadaye huenda Msikitini na kusali pamoja na Liwali wa Kibaniy Umayyah. na kuzifanya Sala zao mbili hizo ni Subha yaani Sunna.

 [1] Hadithi hii imetajwa pia katika Hadithi namba 208.      

[2] Kuombea shari na uovu kwa Mwenyezi Mungu.

[3] Ujeuri (mateso na kudhalilisha).

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment