Ibadhi.com

2. HOJA YA KWA WANAOSEMA IMANI NI KAULI BILA KITENDO.

 

768. A-Rrabi`i bin Habiyb kasema kwamba, "Nimearifiwa kutoka kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«لَعَنَ اللَّهُ الْمُرْجِئَةَ عَلَى لِسَانِ سَبْعِينَ نَبِيًّا قَبْلِي» قِيلَ: وَمَا الْمُرْجِئَةُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «الذِينَ يَقُولُونَ: الإِيمَانُ قَوْلٌ بِلاَ عَمَلٍ».

Maana yake, “Allah amewalani Murji-ah kwa ndimi sabini za Mitume waliokuja kabla yangu". Ikaulizwa: “Na nani hao Murji-ah ewe Mtume wa Mola?” Akajibu: Wale wanaosema kwamba Imani ni kauli bila kitendo”.

 

769. Jaabir bin Zayd kasema, "Wakati Mtume (S.A.W.) alipokuwa amekaa pamoja na Masahaba wake alimijia (mtu mmoja) mwenye uso mzuri na manukato yenye kunukia sana, akasema, "Jee, nikukaribie ewe Mjumbe wa Mola?” Akamjibu, “Ndiyo”. Akamsogelea akamwambia, “Nini maana ya Imani ewe Mjumbe wa Allah (S.A.W.)?, akasema, "

 «أَنْ تُؤْمِنَ بِاللَّهِ وَمَلاَئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ أَنَّهُ مِنَ اللَّهِ»، فَقَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: وَمَا الإِسْلاَمُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «إِقَامُ الصَّلاَةِ وَإِيتَاءُ الزَّكَاةِ وَصِيَامُ شَهْرِ رَمَضَانَ وَالاِغْتِسَالُ مِنَ الْجَنَابَةِ وَحَجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً»، قَالَ: صَدَقْتَ، ثُمَّ تَغَيَّبَ فَإِذَا هُوَ جِبْرِيلُ عَلَيْهِ السَّلاَمُ.

Maana yake, “Ni kuamini (kuwepo kwa) Allah, na Malaika Wake, na vitabu Vyake, na Mitume Wake, na siku ya Mwisho, na kuamini kudra kheri yake, na shari yake ni kutoka kwa Allah”. Akasema, "Umesema kweli”. Akasema, "Na nini Uislamu?” Akajibu: “(Ni) Kusimamisha Sala, na kutoa zaka, na kufunga mwezi wa Ramadhani, na kuoga janaba, na kwenda kuhiji kwa mwenye uwezo”. Akasema, "Umesema kweli”. Kisha akaondoka na kwenda zake, huyo alikuwa Jibriyl (A.S.).   

 

770. A-Rrabi`i bin Habiyb kasema kwamba, "Mtu mmoja alimwuliza Abu Dharr “Nini Imani?” Abu Dharr (R.A.A) akamsomea aya hii, “

{لَيْسَ الْبِرُّ أَن تُوَلُّواْ وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ...} [1]

Maana yake, “Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. [Bali wema ni wa anaye muamini Allah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanaotimiza ahadi yao wanapo hidi, na wanao umilia katika shida na dhara na wakati wa vita]; mpaka kumalizikia kauli, “

{...وَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ}[2]

Maana yake, “Na hao ndio wajilindao[3]”. Yule mtu akamwabia Abu Dharr (R.A.A): “Mimi sikukuuliza kuhusu wema, Abu Dharr (R.A.A.) akasema, "Mtu mmoja alimjia Mtume (S.A.W.) akamwuliza uliyoyauliza kwangu, na Mtume (S.A.W.) akamsomea hizi aya nilizokusomea mimi”.

 

771. Na Mtume (S.A.W.) aliulizwa kuhusu imani akasema, "

«الصَّبْرُ وَالسَّمَاحَةُ».

Maana yake, “Subira na msamaha”.

 

772. Na Mtume (S.A.W.) aliulizwa ni Muumini yupi bora katika imani akasema, "

«أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا».

 Maana yake, “Mbora wao kwa tabia njema”.

 

773. Na Mtume kasema, "

«الإِيمَانُ مِائَةُ جُزْءٍ، أَعْظَمُهَا قَوْلُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى مِنَ الطَّرِيقِ».

Maana yake, “Imani ina sehemu mia, daraja ya juu (ya imani) ni kauli ya “Hapana mungu (anaepaswa kuabudiwa kwa haki) isipokuwa Allah. Na ndogo yake ni kuondosha uchafu njiani”.

 

774. Siku moja Mtume (S.A.W.) aliulizwa kuhusu imani, na alikuwa amelivaa juba lake akalivua kichwani, tena akapiga kwa mkono wake juu kifuani mwake na akasema, "

«الإِيمَانُ هَاهُنَا الإِيمَانُ فِي الْقَلْبِ».

Maana yake, “Imani ni hapa, imani ni katika moyo”.

 

 

775. Mtume (S.A.W.) kasema, "

«مَا آمَنَ مَنْ آمَنَ بِلِسَانِهِ وَلَمْ يَدْخُلِ الإِيمَانُ فِي قَلْبِهِ»

Maana yake, “Hajaamini mwenye kuamini kwa ulimi wake, na wala haikuingia imani moyoni mwake”.  Hadithi hii inaonyesha Imani ni kauli na vitendo, na atakaesema kinyume ya hivi amekufuru kwa kauli yake.[1] Surat Al-Baqarah aya ya 177.

[2] Surat Al-Baqarah aya ya 177.

[3] Wacha Mungu.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment