Ibadhi.com

18. SANDA, NA KUMKOSHA MAITI.

 

471. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "

«عَلَيْكُمْ بِهَذِهِ الثِّيَابِ الْبِيضِ، أَلْبِسُوهَا أَحْيَاءَكُمْ وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ، فَإِنَّهَا خَيْرُ ثِيَابِكُمْ، وَلاَ تُكَفِّنُوهُمْ فِي حَرِيرٍ، وَلاَ مَعَ شَيْءٍ مِنَ الذَّهَبِ، لأَنَّهُمَا مُحَرَّمَانِ عَلَى رِجَالِ أُمَّتِي، وَمُحَلَّلاَنِ لِنِسَائِهَا».

Maana yake, “Shikamaneni na hizi nguo nyeupe. Wavisheni wahai wenu, na wakafinieni maiti wenu. Kwa hakika ni bora ya nguo zenu, wala msiwakafinie kwa nguo ya hariri, wala kitu cha dhahabu. Kwani vimeharamishwa kwa wanaume wa umma wangu. Na vimehalalishwa kwa wanawake wa umati wangu”.

 

472. Na kutokana na njia hiyo hiyo ya Hadithi, pia Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الْمَقْتُولُ فِي الْمَعْرَكَةِ لاَ يُغَسَّلُ، فَإِنَّ دَمَهُ يَعُودُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِسْكًا»

Maana yake, “Aliyeuwawa katika vita (vya Jihadi) hakoshwi. Kwa hakika damu yake itarejea miski siku ya Kiyama”.

Ibn `Abbas (R.A.A) kasema, "Sanda (hununuliwa) kutokana na rasmali (fedha za maiti), kwa kauli ya Mtume (S.A.W.) kwa maiti aliyefariki naye kahudhuria (mauti yake) kasema, "

«كَفِّنُوهُ فِي ثَوْبَيْهِ»

Maana yake, “Mvalisheni sanda katika nguo zake mbili”. Akaongozewa nguo mbili.

 

473. Na kutokana na njia ya Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) alitoa sanda ya binti yake Ummu Kulthum nguo tano”.

 

474. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa (Bibi) Aisha (R.A.A.H.) kasema, "Mtume (S.A.W.) alivalishwa sanda katika nguo tatu nyeupe sahuuliyya[1] hapana ndani yake kanzu, wala kilemba”.

A-Rrabi`i kasema, "(/سَحُوليَّةsahuuliyyah) ni jina la mahali panapoitwa “Sahuulaa,” na pahala hapo ni katika nchi ya Yemen.

 

475. Abu Ubayda kasema, "Nimearifiwa kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn kasema, "Ummu Atiyyah L-Ansariyyah kasema, "Mtume (S.A.W.) alitujia wakati binti yake alipofariki dunia akasema, "

«اِغْسِلْنَهَا ثَلاَثًا أَوْ خَمْسًا أَوْ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ، إِنْ رَأَيْتُنَّ ذَلِكَ بِمَاءٍ وَسِدْرٍ وَاجْعَلْنَ فِي الآخِرَةِ شَيْئًا مِنْ كَافُورٍ، فَإِذَا فَرَغْتُنَّ فَآذِنَّنِي»

Maana yake, “Muosheni mara tatu, au mara tano, au zaidi ya hivyo mkiona inahitajia, kwa maji na majani ya mkunazi. Na mwisho mumuoshe na kafuur, na mkimaliza nijulisheni”. Baada ya kumaliza akaruhusiwa kuingia ndani akatupa shuka yake akasema, "

«أَشْعِرْنَهَا إِيَّاهُ».

Maana yake, “Mfunike nayo vyema”.

Kasema A-Rrabii, “Mfunike nguo (mfano wa kikoi), na kauli yake mfunike nayo ili imstiri”.

 

476. Na kutokana na njia ya Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Haifai kuwekwa maiti ya Mwislamu (asizikwe) baina ya migongo ya watu wake”. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

«اِغْسِلُوا مَوْتَاكُمْ»

Maana yake, “Waosheni maiti zenu”.  Ikawa ni wajibu kuoshwa maiti ya Mwislamu kwa yule atakaehudhuria maiti.[1] Nguo iliyotoka Sahuulaa Yemen.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment