Ibadhi.com

17. VITA KATIKA NJIA YA ALLAH.

 

464. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَقُولُوا لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، فَإِذَا قَالُوهَا عَصَمُوا مِنِّي دِمَاءَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ إِلاَّ بِحَقِّهَا». وَفِي رِوَايَةٍ أُخْرَى: «دِمَاؤُكُمْ وَأَمْوَالُكُمْ عَلَيْكُمْ حَرَامٌ».

Maana yake, “Nimeamrishwa (na Allah) nipigane na watu vita mpaka washuhudie kwamba hapana mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH. Wakitamka hayo, watasalimika kwangu kutokana na uhai wao, na mali yao, isipokuwa kwa haki ya Uislamu. Na katika Hadithi nyingine “Damu yenu na mali yenu kwenu ni haramu”.

 

465. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Aisha (R.A.A.H.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«مَنْ حَمَلَ عَلَيْنَا السِّلاَحَ فَلَيْسَ مِنَّا».

Maana yake, “Atakaetubebea silaha dhidi yetu hayuko na sisi”.

Abu Ubayda kasema, "Amekusudiwa mwenye kubeba kupeleka kwenye nchi ya maadui”.

 

466. Ar-Rrabi`i, kutoka kwa Abi Ayyuub L-Ansaariy kasema, "Nimemsikia Mtume (S.A.W.) akisema. "

«غَدْوَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوْ رَوْحَةٌ خَيْرٌ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ».

 Maana yake, “Atakaetoka mwanzo wa mchana kwenda kupigana Jihad, au akatoka mwisho wa mchana, ni bora kwake kuliko kuchomozewa na jua”.

 

467. Abu Ubayda kasema, "Imenifikia kutoka kwa Abu Qataada kasema, "Tulitoka pamoja na Mtume (S.A.W.) mwaka wa (vita vya) Hunayni, tulipokutana ilikuwa Waislamu wametawanyika. Akasema, "Nikamwona mtu mmoja miongoni mwa makafiri amemkalia mmoja wa Waislamu, yuko tayari kutaka kumuuwa akasema, "Nikamzungukia hata nikamjia nyuma yake nikampiga kwa upanga kwenye mtulinga wa mabega nikaikata ngao yake. Akasema, "Akanigeukia, na akanikamata kwa nguvu mpaka nikanusa harufu ya mauti, kisha yakamshika mauti akaniachia. Halafu nikaondoka nikamsikia Mtume (S.A.W.) akisema, "

«مَنْ قَتَلَ قَتِيلاً لَهُ عَلَيْهِ بَيِّنَةٌ فَلَهُ سَلَبُهُ».

 Maana yake, “Atakayemuuwa mtu, na akawa ana dalili ya kuthibitisha ukweli wake (kuwa aliyeuawa alikuwa na niya ya kuuwa). Basi anaruhusiwa kuchukua silaha zake”. Akasema, "Nikasimama nikasema, "Nani atanishuhudia?” Nikakaa kitako kisha Mtume (S.A.W.) akasema, " “Kama hivyo”. Nikasimama nikasema, "Nani atakenishuhudia?” Baadaye Mtume (S.A.W.) akasema mara ya tatu. Nikasimama. Mtume (S.A.W.) akasema, "

«مَا لَكَ يَا أَبَا قَتَادَةَ»

Maana yake, “Una nini ewe Abu Qatada?”

Nikamhadithia kisa kilichotokea. Mtu mmoja kati ya watu waliokuwapo akasema, "Kasema kweli ewe Mjumbe wa Mola!, Na vifao vyake vya kivita viko kwangu basi mridhie”.

Abu Bakar Siddiyq (R.A.A.) akasema, "La Sivyo hivyo!, Ninaapa kwa Mola hakukusudia kwa aliyekuwa simba katika simba wa Allah, anayepigana kwa ajili ya Mola, na Mtume Wake halafu akupeni ngawira yake. Mtume (S.A.W.) akasema, "

«صَدَقَ فَأَعْطِهِ إِيَّاهُ»

Maana yake, “Kasema kweli, mpeni mwenyewe”.

Abu Qatada kasema, "Akanipa (hivyo vifaa) nikaiuza ngao, fedha nilizopata nikanunua kibustani (chenye mitende michache) kutoka kwa ukoo wa Baniy Salamah, nayo ni mali ya kwanza kumiliki katika Uislamu.

A-Rrabi`i kasema, "(المخِرَف) maana yake ni bustani ya mitende. Na (تَأَثَّلْتُهُ) maana yake ni niliyomiliki/niliyopata.

 

468. Abu Ubayda kasema, "Nilisikia kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) alitoka kwenda Khaybar akafika usiku, na ilikuwa kawaida yake ikiwa atafika kwa watu usiku huwa hawashambulii mpaka kupambazuke. Kulipopambazuka Mayahudi walitoka nje (ya ngome zao) na makoleo yao, na vikapu vyao (wakielekea kwenye mshamba yao). Mara walipomwona Mtume (S.A.W.) wakasema, "Tunaapa kwa Mola, Muhammad na jeshi lake”. Mtume (S.A.W.) akajibu akasema, "

«اللَّهُ أَكْبَرُ خَرَبَتْ خَيْبَرُ إِنَّا إِذَا نَزَلْنَا بِسَاحَةِ قَوْمٍ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنْذَرِينَ».

Maana yake, “Allah Mkubwa, imeharibika Khaibar. Sisi tukishuka uwanja wa watu huwa Asubuhi mbaya kwa wale walioonywa (wasionyeke)”.

 

469. A-Rrabi`i, kutoka kwa Ubaada bin Ssaamit (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) alitusalisha wakapita ngamia waliobeba ngawira. Alipomaliza kusalisha, akamchukua kupe kutoka kwa ngamia akasema, "

«مَا يَحِلُّ لِي مِنْ غَنَائِمِكُمْ مَا يَزِنُ هَذِهِ إِلاَّ الْخُمُسِ وَهُوَ مَرْدُودٌ فِيكُمْ».

Maana yake, “Hainijuzu mimi kuchukua katika ngawira zenu kiasi cha uzito wa huyu kupe, isipokuwa sehemu moja ya tano tu, nayo itarudishwa kwenu”.

Na vita vya Dhaati Ssalaasil vimetajwa katika mlango wa Tayammamu. Na vita vya Dhiy Anmaar vimetajwa katika mlango wa Nguo/Mavazi. Na vita vya Abu Ubaydabin Jarraah vimetajwa katika mlango wa chakula.

 

470. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.) kasema, "Tulitoka pamoja na Mtume (S.A.W.) katika mwaka wa Khaybar hatukuteka dhahabu wala fedha, ila mali, na vifaa. Mtu mmoja wa kabila la Baniy Dhubayb anayeitwa Rufaa`ah bin Zaid alimpa zawadi Mtume (S.A.W.) mtoto mdogo mwenye rangi nyeusi anayeitwa Mid`am. Mtume (S.A.W.) alielekea Wadi Quraa tulipofika, Mid`am, akawa anashusha tandiko juu ya kipando cha Mtume (S.A.W.), mara ukaja mshale usiojulikana wapi unakotoka ukamchoma Mid`am ukamuuwa. Watu wakasema, "Pongezi kwake kwa kuingia Peponi”. Mtume (S.A.W.) akasema, "

«لاَ وَالذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّ الشَّمْلَةَ الَّتِي أَخَذَهَا مِنَ الْمَغَانِمِ يَوْمَ خَيْبَرَ لَمْ تُصِبْهَا الْمَقَاسِمُ لَتَشْتَعِلُ عَلَيْهِ نَارًا».

Maana yake, “La! Naapa kwa Yule nafsi yangu iko mkononi Mwake, hakika nguo ya kujifunika aliyoichukua katika ngawira (bila ruhusa) siku ya (vita vya) Khaybar haikuingizwa katika mgao wa ngawira, itamchoma moto”.

Watu waliposikia hayo mtu mmoja alikuja kwa Mtume (S.A.W.) na kiatu kimoja, au viatu viwili. Mtume (S.A.W.) akasema, "

«شِرَاكٌ أَوْ شِرَاكَانِ مِنَ النَّارِ».

 Maana yake, “Kanda ya kiatu kimoja, au viatu viwili ni za Motoni”.  

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment