Ibadhi.com

16. KUHUSU FARASI

461. Abu Ubayda kasema, "Nimepata khabari itokayo kwa Mtume (S.A.W.) kuwa alishindana baina ya farasi aliyefundishwa (namna ya kushindana) kutoka kijiji kilichoitwa L-Hayfaa, mpaka Thaniyyata L-Widaa`a sehemu ya mwisho ya mashindano. Kisha akashindana kwa farasi ambao hawakupata mafunzo kutoka Thaniyya mpaka kwenye Msikiti wa Bani Ruzaiq. Pia nimearifiwa kwamba Abdullah bin Umar (R.A.A.) alikuwa ameshiriki katika mashindano hayo.

 

462. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A). kasema, "Umar bin Khattaab (R.A.A.) alimbeba mtu mmoja juu ya farasi aliyetolewa kwa ajili ya Allah kwa ajili ya jihad, akamkuta anauzwa sokoni. Akamuuliza Mtume (S.A.W.) juu ya farasi huyo, akamjibu akasema, "

«لاَ تَبْتَعْهُ وَلاَ تَعُدْ فِي صَدَقَتِكَ فَإِنَّ الْعَائِدَ فِي صَدَقَتِهِ كَالْكَلْبِ الْعَائِدِ فِي قَيْئِهِ».

Maana yake, “Usimnunue, wala usirejeshe katika sadaka yako. Kwa hakika anayekirudisha alichokitoa katika sadaka ni kama mbwa aliyetapika, halafu akayala yale  matapishi yake”.

 

463. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الْخَيْلُ لِرَجُلٍ أَجْرٌ وَلِرَجُلٍ سِتْرٌ، وَعَلَى رَجُلٍ وِزْرٌ، فَأَمَّا الَّتِي هِيَ لَهُ أَجْرٌ فَرَجُلٌ رَبَطَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَأَطَالَ لَهَا فِي مَرْجٍ أَوْ رَوْضَةٍ فَمَا أَصَابَتْ فِي طِيَلِهَا ذَلِكَ مِنَ الْمَرْجِ أَوِ الرَّوْضَةِ كَانَ لَهُ حَسَنَاتٍ، وَلَوْ أَنَّهَا قَطَعَتْ طِيَلَهَا ذَلِكَ فَاسْتَنَّتْ شَرَفًا أَوْ شَرَفَيْنِ كَانَتْ آثَارُهَا وَأَرْوَاثُهَا حَسَنَاتٍ لَهُ لَوْ أَنَّهَا مَرَّتْ بِنَهْرٍ فَشَرِبَتْ مِنْهُ وَلَمْ يُرِدْ أَنْ تَشْرَبَ مِنْهُ كَانَ لَهُ ذَلِكَ حَسَنَاتٍ فَهِيَ لَهُ أَجْرٌ؛ وَرَجُلٌ رَبَطَهَا تَغَنِّيًا وَتَعَفُّفًا وَلَمْ يَنْسَ حَقَّ اللَّهِ فِي رِقَابِهَا وَلاَ فِي ظُهُورِهَا فَهِيَ لَهُ سِتْرٌ؛ وَرَجُلٌ رَبَطَهَا فَخْرًا وَرِيَاءًا وَنِوَاءً لأَهْلِ الإِسْلاَمِ فَهِيَ عَلَى ذَلِكَ وِزْرٌ».

Maana yake, “Farasi kwa mtu ni ujira, na farasi kwa mtu mwingine ni stara, na kwa mtu wa tatu ni madhambi. Kwa yule mwenye ujira ni wa mtu yule aliyemtayarisha farasi (wake) katika njia ya Allah, akamfunga kamba, na kumrefushia katika ardhi ya kijani kibichi yenye majani mengi, au bustani. Atakuwa na thawabu kwa yale malisho yake. Na ikiwa atakata kamba hiyo, (kisha huyo farasi) akapiga mbio shoti moja, au shoti mbili, basi athari yake (ya miguu), na kinyesi chake ni thawabu kwake. Na lau kama amepita katika mto akanywa maji yake, na hakuwa na nia ya kumnywesha hayo yote ni thawabu kwake. Huo ndio ujira. Na mtu yule aliyemtayarisha (farasi wake) kwa kujitosheleza mwenyewe, bila kutaka sifa kisha hakusahau haki ya Mola Mtukufu katika shingo yake, wala kumkodisha kwa mwenye kumhitajia, hii kwake ndio stara. Na mtu yule aliyemtayarisha (farasi wake) kwa kujifakharisha, na kujionesha (kwa watu), na kuwafanyia uadui Waislamu, hii ndio dhambi”.

ARrabi`i kasema, "(أَطَالَ لهَا) maana yake ikiwa atamfunga farasi kamba katika ardhi ya kijani kibichi, yenye majani mengi, na kumrefushia kamba kutosha kula majani. Na maana ya (اسْتَنَّتْ) ni kumwachia huru farasi kuruka ruka, na kwenda mbio. Na maana ya (لَمْ يَنْسَ حَقَّ اللَّهِ) ni hakuacha kutoa haki ya Mola (mfano Zaka). Na maana ya (وَنِوَاءً لأَهْلِ الإِسْلامِ) ni kuwafanyia uadui Waislamu".

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment