Ibadhi.com

15. FADHILA ZA KUFA SHAHIDI.

 

452. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.), kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

«وَالذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوَدِدْتُ أَنْ أُقَاتِلَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَأُقْتَلَ، ثُمَّ أُحْيَا ثُمَّ أُقْتَلَ، ثُمَّ أُحْيَا ثُمَّ أُقْتَلَ».

Maana yake, “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake. natamani nipigane katika njia ya Allah halafu niuawe kisha niwe hai, tena nipigane niuwawe, halafu niwe hai, baadaye nipigane niuwawe”.

 

453. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.), kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

«وَالذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لاَ يُكْلَمُ أَحَدٌ فِي سَبِيلِ اللَّهِ - وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَنْ يُكْلَمُ فِي سَبِيلِهِ إِلاَّ جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَجُرْحُهُ يَثْعَبُ دَمًا، اللَّوْنُ لَوْنُ الدَّمِ وَالرِّيحُ رِيحُ الْمِسْكِ».

Maana yake, “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake, haumii yeyote katika njia ya Allah, na Allah hujua aliyeumia katika njia Yake, isipokuwa atakuja siku ya Kiyama na jeraha lake linatiririka damu, na rangi (yake ya ile damu inayotiririka) ni rangi ya damu, na harufu (yake) ni harufu ya miski”.

 

454. Na kwa njia hiyo hiyo kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

«مَثَلُ الْمُجَاهِدِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ كَمَثَلِ الصَّائِمِ الْقَائِمِ الذِي لاَ يَفْتُرُ عَنْ صَلاَةٍ وَلاَ صِيَامٍ حَتَّى يَرْجِعَ».

Maana yake, “Mfano wa mpiganaji katika njia ya Allah, ni kama mfano wa mfungaji aliyesimama akisali, ambaye hapunguzi wala hachoki katika Sala, wala Saumu mpaka arejee”.

 

455. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Kasema Mtume wa Allah (S.A.W.), "

«أَفْضَلُ الأَعْمَالِ كَلِمَةُ حَقٍّ يُقْتَلُ عَلَيْهَا صَاحِبُهَا عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ».

Maana yake, “Bora ya vitendo, ni neno la haki analouliwa nalo mwenye (kulisema) mbele ya mtawala dhalimu.[1]

 

456. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.), kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

«تَكَفَّلَ اللَّهُ لِلْمُجَاهِدِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلاَ يُخْرِجُهُ مِنْ بَيْتِهِ إِلاَّ الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَتَصْدِيقُ كَلِمَاتِهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ، أَوْ يَرُدَّهُ إِلَى مَسْكَنِهِ الذِي خَرَجَ مِنْهُ مَعَ مَا نَالَ مِنْ أَجْرٍ أَوْ غَنِيمَةٍ»

Maana yake, “Allah amechukua dhamana kwa mujahid aliye katika njia ya Allah, ambae hakikumtoa nyumbani kwake ila kwa kufanya jihadi, na kusadikisha neno Lake, basi Mola atamwingiza Peponi, au amrudishe mahali pake alipotokea pamoja na ujira aliyo upata, au ngawira (mali aliyoiteka)”.

 

457. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Alinisimulia Abdullah bin Umar (R.A.A.) kasema, "Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (S.A.W.) akasema, "Ewe Mtume wa Mola (S.A.W.)! “Jee, nikipigana kwa njia ya Mola nikasubiri, nikitegemea kupata malipo, nikasonga mbele bila kurudi nyuma, Allah atanisamehe madhambi yangu?” Akamjibu

«نَعَمْ»

Maana yake, “Ndiyo”. Yule mtu alipoondoka Mtume (S.A.W.) akamwita, akaitiwa (akaja) akasema kumuuliza, "

«كَيْفَ قُلْتَ»

Maana yake, “Ulisema kitu gani?” (Yule mtu) Akayarudia maneno yake (yale aliyoyasema), (Halafu) Mtume (S.A.W.) akasema (kumjibu), "

«نَعَمْ، إِلاَّ الدَّيْنَ، كَذَلِكَ قَالَ لِي جِبْرِيلُ عَلَيْهِ السَّلاَمُ».

Maana yake, “Naam, Utasemehewa isipokuwa deni. Hivi ndivyo alivyoniambia Jibril (A.S.)”.

 

458. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.), kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الْمَقْتُولُ فِي الْمَعْرَكَةِ لاَ يُغَسَّلُ، فَإِنَّ دَمَهُ يَعُودُ مِسْكًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ».

Maana yake, “Anayeuwawa katika vita (vya jihadi) hakoshwi. Kwani damu yake inageuka miski siku ya Kiyama”.

 

459. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema kuhusu waliokufa mashahidi. "

«زَمِّلُوهُمْ فِي ثِيَابِهِمْ»

Maana yake, “Wafunikeni katika nguo zao (walizofia)”.

 

460. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«لَوْلاَ أَنْ أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي لأَحْبَبْتُ أَنْ لاَ أَتَخَلَّفَ عَنْ سَرِيَّةٍ تَخْرُجُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، وَلكِنْ لاَ أَجِدُ مَا أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ وَلاَ تَجِدُونَ مَا تُحْمَلُونَ عَلَيْهِ، وَيَشُقُّ عَلَيْكُمْ أَنْ تَتَخَلَّفُوا بَعْدِي».

Maana yake, “Kama nisingeliuonea taabu (na huruma) umma wangu nisingelipenda kubaki nyuma kutokufuatana na kundi la jeshi linalotoka kwenda kupigana katika njia ya Allah. Lakini sina kipando cha kukuchukueni, na wala nyie hamna kipando cha kukuchukueni. Na ikawa dhiki kwenu msije mkakengeuka baada (ya kufa) kwangu”.[1] Mfano wa Hadithi hii imetolewa katika Hadithi namba 448.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment