Ibadhi.com

14. AINA ZA MASHAHIDI.

 

448. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الْمَقْتُولُ دُونَ مَالِهِ شَهِيدٌ».

Maana yake, “Aliyeuawa akitetea asinyang’anwe mali yake ni shahidi”.  Vilevile akasema, "

«أَفْضَلُ الأَعْمَالِ كَلِمَةُ حَقٍّ يُقْتَلُ عَلَيْهَا عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ».

Maana yake, “Bora ya kitendo ni neno la haki kuuliwa nalo mwenye kulisema mbele ya kiongozi dhalimu (asiyehukumu kwa sheria)”.

 

449. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الشُّهَدَاءُ خَمْسَةٌ: الْمَطْعُونُ، وَالْمَبْطُونُ، وَالْغَرِيقُ، وَصَاحِبُ الْهَدَمِ، وَالشَّهِيدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ».

Maana yake, “Mashahidi ni (wa aina) tano: Aliyekufa kwa maradhi ya tauni, na kwa maradhi ya tumbo, na aliyezama ndani ya maji, na mwenye kuangukiwa (na nyumba au mchimba kisima akangukiwa na udongo), na shahidi aliyekufa katika njia (ya kupigania dini) ya Allah”.

 

450.A-Rrabi`i kasema, "Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الشَّهِيدُ يُغْفَرُ لَهُ عِنْدَ أَوَّلِ قَطْرَةٍ تَقْطُرُ مِنْ دَمِهِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، وَيُجَارُ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ».

Maana yake, “Aliyekufa shahidi husamehewa makosa yake, wakati linapodondoka tone la mwanzo la damu yake katika njia ya Allah. Na ataepushwa na mateso ya kaburini”.

 

451. Na Mtume (S.A.W.) kasema, "

«إِنْ لَمْ يَكُنِ الشُّهَدَاءُ مِنْ أُمَّتِي إِلاَّ مَنْ قُتِلَ بِالسَّيْفِ فَهُمْ إِذَنْ قَلِيلٌ»

Maana yake, “Ingelikuwa mashahidi katika umma wangu hawapatikani isipokuwa kwa kuuwawa kwa upanga wangekuwa wachache”. Kisha Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الْقَتِيلُ شَهِيدٌ وَصَاحِبُ الْهَدَمِ شَهِيدٌ، وَالْمَبْطُونَ شَهِيدٌ، وَالْغَرِيقُ شَهِيدٌ، وَمَنْ أَكَلَهُ السَّبُعُ شَهِيدٌ، وَالسَّلِيمُ شَهِيدٌ - يَعْنِي اللَّدِيْغَ - وَصَاحِبُ السِّلِّ شَهِيدٌ، وَمَنْ مَاتَ مُرَابِطًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَمَنْ ذَكَرَ اللَّهَ تَعَالَى إِذَا أَخَذَ مَضْجَعَهُ ثُمَّ مَاتَ فَهُوَ شَهِيدٌ، وَالنُّفَسَاءُ وَمَنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ يُرِيدُ أَنْ تَكُونَ كَلِمَةُ اللَّهِ هِيَ الْعُلْيَا وَكَلِمَةُ الذِينَ كَفَرُوا السُّفْلَى شَهِيدٌ».

Maana yake, “Aliyeuwawa (katika vita vya Jihadi) ni shahidi, na mwenye kuporomokewa (na nyumba au ukuta n.k) ni shahidi, na aliyekufa kwa maradhi ya tumbo ni shahidi, na anayekufa kwa kugharikika (kuzama katika maji) ni shahidi, na atakayekufa kwa kuliwa na mnyama ni shahidi, na atakayekufa katafunwa na mdudu (nyoka, nge n.k) ni shahidi, na mwenye kufa kwa kifua kikuu ni shahidi, na aliyekufa ameshikamana katika njia ya Allah ni shahidi, na atakayekufa anamtaja (anamdhukuru) Mola akilala kitandani kwake kisha akafa ni shahidi, na mwanamke aliyekufa akizaa ni shahidi, atakayekufa  kitandani kwake nae ameazimia[1] kulifanya neno la Allah kuwa ndilo juu, na neno la waliokufuru kuwa chini ni shahidi”.[1] Amekusudia.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment