Ibadhi.com

13. KUFUNGAMANA (KIAPO CHA KUTII) (البَيْعَةُ)

 

445. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kasema, "`Ubaada bin Ssaamit kasema, "Tuliاchukua ahadi kwa Mtume (S.A.W.) kumsikiliza, na kumtii wakati wa shida, na wakati wa raha, kwa yanayochukiza, na kwa yanayopendeza, na kutowapinga wale waliopewa madaraka juu yetu, (wale wenye kushikamana na amri ya Mola), na tuseme haki, na tusimamishe haki popote pale tulipo. Na bila kuogopa lawana kwa ajili ya Mola”.

 

446. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Umar (R.A.A.) kasema, "Tulichukua ahadi kwa Mtume (S.A.W.) kumsikiliza, na kumtii na akasema, "

«فِيمَا اسْتَطَعْتُمْ».

Maana yake, “Kwa yale mnayoyaweza”.

Jaabir kasema, "Na nimesikia kwa Sahaba waliokuwa wakisema, “Wameahidi wasikimbie”.

 

447. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Nilimsikia Jaabir bin Abdullah akisema, “Bedui alifunganiana ahadi na Mtume (S.A.W.), (halafu) yule Bedui akapatwa homa kali wakati alipokuwepo Madina akasema, "Ewe Mtume (S.A.W.)! Itengue ahadi yetu, lakini Mtume (S.A.W.) alimkatalia. Akamjia mara ya pili, na ya tatu, akamkatalia. Bedui akatoka akaenda zake, Mtume (S.A.W.) akasema, "

«إِنَّمَا الْمَدِينَةُ كَالْكِيرِ تَنْفِي خَبَثَهَا وَتُمْسِكُ طَيِّبَهَا».

Maana yake, “Hakika (mji wa) Madina ni kama kiriba cha kupulizia moto, huondosha wabaya wake na kuzuia wazuri wake”.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment