Ibadhi.com

12. FADHILA ZA HAJI NA `UMRA.

 

443. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«الْعُمْرَةُ إِلَى الْعُمْرَةِ كَفَّارَةٌ لِمَا بَيْنَهُمَا، وَالْحَجُّ الْمَبْرُورُ لَيْسَ لَهُ جَزَاءٌ إِلاَّ الْجَنَّةُ».

Maana yake, “Umra mpaka Umra ni kafara ya baina yake, na Hajji iliyotimizwa kikamilifu na kukubaliwa haina malipo isipokuwa ni Pepo”.

 

444. Abu Ubayda kutoka, kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa (Bibi) Aisha (R.A.A.H.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«اللَّهُمَّ ارْحَمِ الْمُحَلِّقِينَ»

Maana yake, “Ewe Mola! Warehemu wanaonyoa (nywele zao katika Umra au Hijja)”.

Wakasema, "Ewe Mtume (S.A.W.) na wanaopunguza (nywele zao)?" Akasema, "

«وَالْمُقَصِّرِينَ».

Maana yake, “Na wanaopunguza (nywele zao)”.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment