Ibadhi.com

10. KUWINDA KWA ALIYEKUWA MUHRIM.

 

 436. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtu mmoja (aliyeitwa Ssa`abu bin Jaththaama) alimpa Mtume (S.A.W.) zawadi ya punda wa mwituni walipo kuwa Al-Abwa. Lakini  Mtume (S.A.W.) akamrejeshea mwenyewe (punda wake). Alipoona Mtume (S.A.W.) alama ya kutokupendezewa katika uso wake akasema, "

«إِنَّا لَمْ نَرُدَّهُ عَلَيْكَ إِلاَّ أَنَّا مُحْرِمُونَ»

Maana yake, “Sisi hatukukurejeshea isipokuwa tumehirimia”.

 

437. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) alitoka kuelekea Makka naye akiwa amehirimia hata alipofika mahali panapoitwa Rrawhaa alipambana na punda wa mwituni aliyejuruhiwa, Mtume (S.A.W.) akasema, "

«دَعُوهُ يُوشِكُ أَنْ يَأْتِيَهُ صَاحِبُهُ».

Maana yake, “Mwachieni mwenyewe hayuko mbali atakuja sasa hivi”.

Akaja L-Bahziyyi (Zaid bin Ka`ab Aslimiy) naye ndiye akiwa mwenye punda akasema, "Ewe Mtume wa Allah (S.A.W.) mfanyeni mtakavyo punda huyu”. Mtume (S.A.W.) akamwamrisha Abu Bakar (R.A.A.) amgawe. Akamgawa miongoni mwa wale aliofuatana nao. Halafu wakaondoka mpaka walipofika Al-Athaaya baina ya Rruwaitha na L-`Araj, wakamwona paa kichwa chake kakiinamisha (kakaa) kivulini anao mshale (mwilini mwake). Mtume (S.A.W.) akamwamrisha mtu mmoja amwangalie asidhuriwe na yeyote mpaka wote wampite.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment