Ibadhi.com

9.TAMAT-TU, IFRAADU, QIRAANU NA RUHUSA.


433. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Aliniarifu Sa`ad bin Abi Waqqaas (R.A.A.),  na Dhihaak bin Qais (R.A.A.) ya kwamba, "Walitofautiana katika kujistarehesha kwa kufanya Umra (kwanza pekee yake) kisha ndio akahiji”. Dhihaak akasema, "Hafanyi hivyo ila yule asiyeelewa amri ya Mola”. Sa`ad akasema, "Ubaya ulioje ulivyosema hivyo”. Dhihaak akasema, " “Hakika `Umar bin Khattaab (R.A.A.) alikataza kufanya hivyo”. Sa`ad akasema, "Mtume (S.A.W.) alifanya hivyo na tukafanya pamoja naye”.

ARrabi`i kasema, "Kasema Ubu Ubayda, “Mwenye kutaka kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji afanye, na atakae aache. Kwani yote hayo ni wasaa[1] uliyo mkubwa”.

 

434. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa (Bibi) Aisha (R.A.A.H.) kasema, "Mtume (S.A.W.) alifanya Hijja peke yake (bila ya kuchanganya na Umra)”.

 

435. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abdullah bin Amrou bin L-`Aas (R.A.A.) kasema, "Katika Hijja ya mwisho (ya Mtume (S.A.W.), mtu mmoja alikuja kwa Mtume (S.A.W.) akasema, "Ewe Mtume wa Mola (S.A.W.)! Sikujua nimenyoa kabla ya kuchinja”. Akamwambia: “Chinja wala hapana kitu”. Akamjia mwingine akamwambia: “Ewe Mjumbe wa Allah (S.A.W.)! Sikujua nimechinja kabla ya kutupa mawe”. Akamwambia: “Chinja wala hapana kitu”. Siku hiyo hakuulizwa kitu chochote ila kasema, "Wala hapana kitu".

ARrabi`i kasema, "Hii ruhusa kutoka kwa Mtume kwa (S.A.W.) ilikuwa ni kwa siku hiyo (tu ya Hijja ya mwisho)”.[1] Ruhusa pevu.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment