Ibadhi.com

8. KICHINJO CHA UDH`HIYA, NA MALIPO KWA MAKOSA NA FIDYA

427. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema, "Ziad bin Abu Sufiyan aliandika barua kumpelekea (Bibi) Aisha mama wa Waislamu (R.A.A.H.) akamuelezea kuwa Abdullah bin Abbas (R.A.A.) anasema, “Yanamharamikia mwenye kupeleka mnyama wa kutolewa sadaka (wakati wa Hija), kama yanavyomharamikia mwenye kuhiji mpaka achinjwe yule mnyama, nami nimempeleka mnyama wangu basi niandikie kwa amri yako”. (Bibi) Aisha (R.A.A.H.) kasema, "Si kama alivyosema Ibn Abbas (R.A.A.), kwani mimi nilifungua kamba ya shingoni ya mnyama wa kuchinjwa wa Mtume (S.A.W.) kwa mkono wangu, kisha yeye akamfunga kamba, halafu akampeleka kwa baba yangu, wala hakuharamisha Mtume (S.A.W.) kitu alichomhalalishia Allah mpaka amchinje mnyama wake”.

 

428. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema, "Hafsa (R.A.A.H.) kasema kumwambia Mtume (S.A.W.), “Mbona watu wameshatahallal[1] lakini wewe bado hujat`halal[2] kwa Umra yako?” Akasema, "

«إِنِّي لَبَّدْتُ رَأْسِي وَقَلَّدْتُ هَدْيِي فَلاَ أَحِلُّ حَتَّى أَنْحَرَ».

Maana yake, “Hakika mimi nimetia kichwani kitu kinachozuia nywele zangu, na nimemtia mnyama wangu alama shingoni siwezi kutahallal mpaka nichinje”.

Arabi`i kasema, "(التَّلبيد) maana yake ni kitu kinachozuia nywele zisitawanyike”.

 

429. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.) ya kuwa, "Mtume (S.A.W.) alimwona mtu mmoja anamvuta ngamia jike, akamwambia,

«اِرْكَبْهَا»

Maana yake, "Mpande (mkwee)!". Akasema, "Ewe Mtume (S.A.W.)! Huyu ni ngamia jike". Akamwambia, "

«اِرْكَبْهَا»

Maana yake, "Mpande (mkwee)". Akasema, "Huyu ni ngamia jike”. Mtume (S.A.W.) akasema, "

«اِرْكَبْهَا وَيْلَكَ»

Maana yake, “Ole wako! Mkwee,” kwa mara ya pili au ya tatu”.

 

430. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Jaabir bin Abdullah kasema, "Tulichinja pamoja na Mtume (S.A.W.) katika mwaka wa Hudaybia. Ngamia jike kwa ajili ya watu saba, na ngombe jike kwa ajili ya watu saba".    

 

431. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa (Bibi) Aisha mama wa Waislamu (R.A.A.H.) kasema, "Tulifuatana pamoja na Mtume (S.A.W.) kwa masiku matano yaliyobakia katika Dhul-Qa`ida (mwezi wa mfungo pili) wala hatukuona isipokuwa L-Hajji (mwezi wa mfungo tatu). Na tulipokaribia Makka Mtume (S.A.W.) alimuamrisha kila asiyekuwa na ngamia wa kuchinja, akitufu (akizunguka) L-Ka`aba, na akatembea baina Safaa na Marwaa, basi atanyoa nywele. Seyyida Aisha (R.A.A.H.) kasema, "Tukaletewa nyama ya ng`ombe siku ya kuchinja, nikauliza, “Kwa ajili gani hii nyama?” Akajibu, “Mtume (S.A.W.) kachinja kwa ajili ya wake zake”.

  

432. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Ka`ab bin Ujra alitoka pamoja na Mtume (S.A.W.) kwa ajili ya kuhiji, lakini aliudhiwa na chawa kichwani mwake. Mtume (S.A.W.) alimwamrisha anyoe nywele zake, na akamwambia, "

«صُمْ ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ، أَوْ أَطْعِمْ سِتَّةَ مَسَاكِينَ مُدَّيْنِ لِكُلِّ مِسْكِينٍ، أَوْ اُنْسُكْ بِشَاةٍ أَيَّ ذَلِكَ فَعَلْتَ أَجْزَاكَ».

Maana yake, “Funga siku tatu, au walishe maskini sita kila maskini vibaba viwili, au toa sadaka kwa kuchinja mbuzi mmoja. Ukifanya mojawapo katika haya (mambo matatu) itatosheleza”.[1] Wameshatoka katika vitendo vya umra. Na hii inakuwa aghlabu kwa kunyoa nywele au kuzikata.

[2] Hujatoka kwa kumaliza vitendo vya umra.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment