Ibadhi.com

7. YANAYOHSU `ARAFA, NA MUZDALAFA NA MINA

 

420. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Sa`id L-Khudriyy (R.A.A.) kasema, "Watu walitofautiana walipokuwa kwa Ummu L-Fadhl bint L-Haarith, naye ni mama mzazi wa Abdullah bin Abbas (R.A.A.) kuhusu Mtume (S.A.W.) kama kafunga siku ya Arafah, wako walio sema kwamba yeye kafunga, wengineo wakasema hakufunga, akasema Abu Said, "Ummu L-Fadhl akampelekea Mtume (S.A.W.) kibakuli cha maziwa, naye amesimama juu ya ngamia wake akayanywa”.

 

421. Abu Ubayda kasema, "Niliarifiwa na Usaamah bin Zaid (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) aliondoka Arafah hata alipowasili Ash-sha`ab, akateremka kwenda haja ndogo, halafu akatawadha, lakini hakuutengeneza udhu wake nikwambia, “Wakati wa Sala umefika”. Akajibu akasema,

«الصلاة أماماك».

Maana yake, “Sala iko mbele yako”. (Halafu) Akapanda kwenye kipando chake. Walipowasili Muzdalifa, akateremka akatawadha, akautengeneza udhu wake, kisha pakakimiwa Sala, akasali Sala ya Magharibi. Kisha kila mtu akamfunga ngamia wake, nyumbani kwake, baadaye pakakimiwa Sala ya Isha, akaisali, wala hakuzitenganisha baina ya Sala hizo mbili kwa kitu chochote kile”.

ARrabi`i kasema, "Abu Ubayda kasema, "Inapendeza baada ya (Sala ya) Magharibi (kuzisali) rakaa mbili zilizokuwa hafifu (nyepesi)”.

 

422. Abu Ubayda kasema, "Allah Mtukufu alipomruhusu Mtume Wake (S.A.W.) kuhiji Hija ya kuaga, nayo ni hija iliyokamilika akasimama Arafah akasema, "

«أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ الزَّمَانَ قَدِ اسْتَدَارَ كَهَيْئَةِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ، فَلاَ شَهْرَ يُنْسَى، وَلاَ عِدَّةَ تُحْصَى، أَلاَ وَإِنَّ الْحَجَّ فِي ذِي الْحِجَّةِ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ».

Maana yake, “Enyi watu! Hakika wakati umegeuka kama mfano wa siku Allah alipoziumba mbingu na ardhi, hapana siku za mwezi kusahauliwa, wala idadi ya siku zinazohesabika, jueni ya kwamba Hija hufanyika mnamo mwezi wa Dhul Hijja (mfungo tatu) mpaka siku ya Kiyama”.  Abu Ubayda kasema, "Alipotimiza Hija yake akawahutubia huko Arafah akasema, " 

«إِنَّ أَهْلَ الشِّرْكِ وَالأَوْثَانِ كَانُوا يَدْفَعُونَ مِنْ عَرَفَاتٍ إِذَا صَارَتِ الشَّمْسُ عَلَى رُؤُوسِ الْجِبَالِ كَأَنَّهَا عَمَائِمُ الرِّجَالِ فِي وُجُوهِهِمْ، وَيدْفَعُونَ مِنَ الْمُزْدَلِفَةِ إِذَا طَلَعَتِ الشَّمْسُ عَلَى رُؤُوسِ الْجِبَال كَأَنَّهَا عَمَائِمُ الرِّجَالِ فِي وُجُوهِهِمْ، وَإِنَّا لاَ نَدْفَعُ مِنْ عَرَفَاتٍ حَتَّى تَغْرُبَ الشَّمْسُ، وَيُفْطِرَ الصَّائِمُ، وَنَدْفَعُ مِنَ الْمُزْدَلِفَةِ غَدًا إِنْ شَاءَ اللَّهُ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ، هَدْيُنَا مُخَالِفٌ لِهَدْيِ أَهْلِ الشِّرْكِ وَالأَوْثَانِ».

Maana yake, “Hakika washirikina, na wenye kuabudu masanamu walikuwa wakiondoka Arafaat, wakati jua limepanda juu ya vichwa vya majabali (vileleni) utadhania mfano wa kama vilemba vya wanaume ndani ya nyuso zao. Na wanaondoka Muzdalifa linapochomoza jua juu ya vichwa vya majabali (vileleni), utadhania mfano wa kama vilemba vya wanaume ndani ya nyuso zao. Na sisi hatuondoki Arafaat mpaka lichwe jua, na afuturu mtu aliyefunga. Na kesho tutatoka kutoka Muzdalifa akipenda Allah kabla ya jua halijachomoza. Uwongofu wetu ni tofauti na uwongofu wa washirikina, na wenye kuabudu masanamu”.

 

423. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Aliulizwa Usaamah bin Zaid (R.A.A.) namna gani Mtume Wake (S.A.W.) alipokuwa akienda kufanya Hija ya mwisho wakati wa kuondoka?” Akajibu akasema, "Alikuwa akienda kwa haraka sana, na akikuta pahala penye kukaa sawa humharakisha mnyama ili aende kwa haraka zaidi”.

 

424. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Nimearifiwa kuwa Abuu Ayuub al Ansariy Sahaba wa Mtume (S.A.W.) kasema, "Nilisali na Mtume (S.A.W.) wakati wa Hija ya widaa Sala ya Magharibi na Sala ya Isha pamoja tulipokuwa Muzdalifa.

 

425. Abu Ubayda kasema, "Nimepata habari kutoka kwa Ibn `Umar (R.A.A) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«إِذَا كُنْتَ بَيْنَ الأَخْشَبَيْنِ بِمِنًى - وَنَفَخَ بِيَدِهِ نَحْوَ الْمَشْرِقِ - فَإِنَّ هُنَاكَ وَادِي السُّرَرِ فِيهِ سَرْحَةٌ سُرَّ تَحْتَهَا سَبْعُونَ نَبِيئًا»

Maana yake, “Utakapokuwepo baina ya majabali mawili katika Mina akaashiria kwa mkono wake kuelekeza upande wa Mashariki. Huko liko bonde linaloitwa Ssuraru (yaani vitovu, panapokatiwa watoto wachanga vitovu vyao, na ndani yake kuna mti mkubwa kabisa), vimekatwa chini yake vitovu vya Mitume sabini”.

 

426. Abu Ubayda kasema, "Mtume (S.A.W.) amewaruhusu wachunga ngamia kulala kwenye makaazi walipofikia, na kutupa mawe siku ya kuchinja, halafu tena kutupa mawe kesho yake, na halafu baada ya kesho yake wanatupa siku mbili, mwishowe wanatupa siku ya kuondoka (kutoka Mina ambayo ni siku ya tatu ya Tashriyq)”.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment