Ibadhi.com

5. YANAYOMPASA KUJIEPUSHA ALIYE HIRIMIA, NA YASIYOMPASA.

 406. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Sa`id L-Khudriyy (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "

«لاَ يَلْبَسُ الْمُحْرِمُ الْقَمِيصَ وَلاَ الْعِمَامَةَ وَلاَ السَّرَاوِيلاَتِ وَلاَ الْبَرَانِسَ وَلاَ الْخِفَافَ، فَإِنْ لَمْ يَجِدْ نَعْلَيْنِ فَلْيَلْبَسْ خُفَّيْنِ، وَلْيَقْطَعْهُمَا مِنْ أَسْفَلِ الْكَعْبَيْنِ»

Maana yake, “Muhrim asivae shati, wala amama[1], wala suruali, wala kofia, wala khuffu[2]. Asipopata makubazi[3] mawili, basi avae khuffein za ngozi na avikate chini ya viwiko vya miguu miwili”. (Pia) kasema (Mtume S.A.W.), "

«وَلاَ يَلْبَسُ الْمُحْرِمُ شَيْئًا مِنْ ثِيَابٍ مَسَّهَا الزَّعْفَرَانُ وَلاَ الْوَرْسُ».

Maana yake, “Muhrim asivae nguo zilizotiwa zaafarani, wala manukato ya maua ya warsi (mfano wa nargisi au mshembeli[4])”.

 

407. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Aisha mke wa Mtume (S.A.W.) kasema, "Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«خَمْسٌ مِنَ الدَّوَابِّ لَيْسَ عَلَى الْمُحْرِمِ فِي قَتْلِهِنَّ جُنَاحٌ: الْغُرَابُ وَالْحِدَأَةُ وَالْفَأْرَةُ وَالْعَقْرَبُ وَالْكَلْبُ الْعَقُورُ».

Maana yake, “Aina tano ya wadudu/wanyama hana makosa Muhrim kuwauwa: Kunguru, na ndege mbaya (aina ya kipanga au furukombe), panya, nge, na mbwa anayejeruhi na kuudhi[5]”.

 

408. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) aliingia Makka mnamo mwaka wa ufunguzi, na juu ya kichwa chake ngao ya chuma, alipoivua akamuijia mtu mmoja akamwambia, “Ewe Mjumbe wa Mola, Ibn Khatal ananing`inia kwenye pazia la L-Ka`aba akasema “Muuweni”. Jaabir kasema, "Nilipewa khabari kwamba Mtume (S.A.W.) siku hiyo hakuhirimia”. [1] Aina fulani ya kitambaa kama kilemba kinachovaliwa kichwani aghalabu kinakuwa na urefu wa karibu dhiraa 18.

[2] Viatu au soksi vinavyofunika kisigino chote na vidole kwa mbele.

[3] Ndara au kandambili au mfano wa hivyo

[4] Aina za mimea zinazotoa harufu inayonukia.

[5] Aghalabu anakuwa ni yule mbwa aliepata kichaa cha mbwa.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment