Ibadhi.com

4. KUKOGA KWA ALIYE HIRIMIA.

 

403. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A) kasema, "Muhrim[1] anakoga kwa maji na majani ya mkunazi”.

 

404. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "

«إِذَا مَاتَ الْمُحْرِمُ غُسِلَ وَلاَ يُكَفَّنُ إِلاَّ فِي ثَوْبَيْهِ اللَّذَيْنِ أَحْرَمَ فِيهِمَا، وَلاَ يُمَسُّ بِطِيبٍ وَلاَ يُخَمَّرُ رَأْسُهُ».

Maana yake, “Akifa Muhrim[2] hukoshwa, wala havikwi sanda ila katika nguo zake mbili ambazo amehirimia nazo, wala hagusishwi manukato, na wala hafunikwi kichwa chake”.

 

405. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Tulitofautiana mimi na Miswar bin Makhrama tukiwa L-Abwaa, nilisema, “Muhrim hukikosha kichwa chake, yeye akasema hakikoshi”. Basi Ibn `Abbas (R.A.A.) akasema, "Nilimtuma mtu mmoja anayeitwa Abdullah bin Hunayn kwenda kwa Abi Ayyuub L-Ansaariy (R.A.A.), akakumkuta anakoga kati ya pembe mbili, naye amejisitiri kwa nguo moja, akamsalimia, halafu akamuuliza, “Nani huyu?” Yule mtu akajibu akasema, "Mimi ni mjumbe niliyetumwa na Ibn Abbas (R.A.A.) ili nije kwako kukuuliza, “Vipi Mtume (S.A.W.) alikuwa akikoga naye ni muhrim?” Yule mtu akasema, "(Abi Ayyuub L-Ansaariy) Akauweka mkono wake juu ya nguo akainama inama mpaka kikanidhihirikia kichwa chake, kisha akamwambia yule mtu anayemmiminia maji, nimwagie, akamwagia juu ya kichwa chake, kisha akayaeneza (maji) kwa mkono wake, mbele na nyuma halafu akasema, "Hivi ndivyo nilivyomwona Mtume (S.A.W.) akifanya”.

Rrabi`i kasema, "(القرنان) ni nguzo mbili zilizopo kwenye jabali la L-Abwaa, kando ya kisima zinateleza ukizishika”.  

 [1] Aliehirimia kwa Hajj au Umra.

[2] Aliehirimia kwa Hajj au Umra.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment