Ibadhi.com

3. KUTOKANA NA IHRAMU YA HIJA NA TALBIYA.

 

399. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Sa`id L-Khudriyy (R.A.A.) kasema, "Talbiya ya Mtume (S.A.W.) ni kusema, "

«لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ  لاَ شَرِيْكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لاَ شَرِيكَ لَكَ»

Maana yake, “Labbayka Llaahumma Labbayka, Labbayka la shariyka Laka labbayka, innal Hamda wanni`imata Laka wal-Mulka la shariyka Laka”. [Nimekuitikia Mola wangu, nimekuitikia, huna mshirika, nimekuitikia. Hakika himidi[1] na neema ni zako pamoja na ufalme, Huna Mshirika]  

Naafi`i kasema, "Ibn `Umar (R.A.A.) alikuwa akizidisha akisema:

لَـبَّيْكَ وَسَعْدَيْكَ، وَالْخَيْرُ بِيَدَيْكَ، وَالرَّغْبَةُ إِلَيْكَ وَالْعَمَلُ.

Maana yake, “Labbayka wasa`adayka wal-khayru biyadayka Labbayka warraghbatu ilayka wal`amalu”. Nimekuitikia Mola Wangu, Na nina kuridhisha tena na tena bila mfano, Na kheri zote Ziko katika mikono Yako, na Natamania, Nakutaka yaliyoko Kwako na kitendo kwa ajili Yako[2].

 

400. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Sa`id L-Khudriyy (R.A.A.) ya kwamba, Mjumbe wa Allah (S.A.W.) wakati anapoondoka kwenda Hijja, au vitani, au Umra hupiga takbira mara tatu kila anapopanda mwinuko wa ardhini (kilima), kisha husema, "

«لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ سَاجِدُونَ عَابِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ، وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ».

 [La ilaaha illa Llaahu wahdahu la shariyka Lahu, Lahu L-Mulku wa-Lahu L-Hamdu wahuwa `ala kulli shay-in qadiyrun. `Aayibuwna taa-ibuwna saajiduwna `aabiduwna lirabbina haamiduwna sa-daqa Llaahu wa`adahu wanasara `abdahu wahazamal ahzaaba wahdahu]”. Maana yake, “Hapana anaepaswa kuabudiwa kwa haki ila Allah peke yake, hana Mshirika. Ufalme ni Wake, na Yeye ndie anaepaswa Kushukuriwa, Naye Muweza wa kila kitu. Tunarejea kwako, na tunatubu, wenye kusujudu, wenye kuabudu, na Mola wetu tunamshukuru. Ametekeleza Allah ahadi yake, na Akamnusuru mja Wake, na Akayashinda makundi ya makafiri peke yake”.

 

401. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Mtu mmoja alikuja kwa Abdullah bin Umar (R.A.A.) akasema, "Baba wa Abdu Rahmaan nimekuona ukifanya mambo manne ambayo sijapata kumwona mmoja wa Masahaba wenzako akiyafanya. Akauliza akasema, "Yapi hayo?” Akajibu akasema, "Nimekuona hugusi pembe ya Al`Kaaba ila pembe ya L-Yamaani, na nimekuona unavaa viatu visivyo kuwa na manyoya, na nimekuona unapaka (nywele zako kwa) rangi ya manjano, na nimekuona unapokuwa Makka watu wanashangilia kwa Tahliyl[3]  wanapouona mwezi, wala hukusema hivyo isipokuwa siku ya Tar-wiya[4]. Ibn Umar akamwambia, "Ama kuhusu pembe, sijawahi kumwona Mtume (S.A.W.) akigusa ila (pembe ya) L-Yamaani. Na ama kuhusu viatu visivyokuwa na manyoya, nimemuona Mtume (S.A.W.) akivaa. Na ama kuhusu kupaka rangi ya manjano, nimemuona Mtume (S.A.W.) akipaka. Ama kuhusu Tahliyl sijawahi kumwona Mtume (S.A.W.) akisema hivyo mpaka kipando chake cha usafiri kimfikishe anapokwenda”.       

 

402. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid kasema, "Mohammad bin Abi Bakar (R.A.A.) alifuatana na Anas bin Maalik (R.A.A.) kutoka Mina mpaka Arafaat. Akamwambia Mohammad bin Abi Bakar (R.A.A.), “Mnafanya nini siku kama hii mnapokuwa pamoja na Mtume (S.A.W.), akajibu akasema, "Anahaliyl miongoni mwetu mwenye kuhaliyl na wala hakatazwi, na anakabir anaepiga takbiyr[5] na wala hakatazwi".[1] Shukrani zote, na sifa zote njema, na utukufu wote.

[2] Kwako wewe ndio makusudi ya ibada zote.

[3] Kwa kusema “La ilaaha illa Llaah".

[4] Hii ni siku ya tarehe 8 ya Dhul-Hijja, siku ya kwanza wanayokutanika Munna kwa kuelekea Arafat.

[5] Kumtukuza Allah kwa kusema Allah Akbar.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment