Ibadhi.com

2. MIQAAT (VITUO VYA HIJA VYA KUHIRIMIA) NA KUHIRIMIA.

 

396. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Sa`id L-Khudriyy (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) alipambanua mpaka wa watu wa Madina Dhi Hulaifa, na watu wa Shamu Juhfa, na watu wa Najdi Qarn L-Manaazil, na watu wa Yemen Yalamlam, na watu wa Iraq Dhati `Irqi.

 

397. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kwamba Mjumbe wa Allah (S.A.W.) alipanda juu ya jabali la Uhud akasema, "

«هَذَا جَبَلٌ يُحِبُّنَا وَنُحِبُّهُ، اللَّهُمَّ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ حَرَّمَ مَكَّةَ وَأَنَا أُحَرِّمُ مَا بَيْنَ لاَبِتَيْهَا».

Maana yake, “Hili ni jabali linatupenda na tunalipenda. Ewe Allah! Hakika Ibrahim ameifanya Makka mahali patakatifu. Nami napafanya mahala hapa patakatifu baina ya mawe yake meusi (milima iliyotokana na volcano). (Makusudio ni mji wa Madina)”.

 

398. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kasema, "Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«مَكَّةُ حَرَامٌ حَرَّمَهَا اللَّهُ، لاَ تَحِلُّ لُقْطَتُهَا، وَلاَ يُعْضَدُ شَجَرُهَا، وَلاَ يُنَفَّرُ صَيْدُهَا، وَلاَ يُخْتَلَى خَلاَهَا». فَقَالَ عَمُّهُ العَبَّاسُ: إِلاَّ الإِذْخِرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَقَالَ: «إِلاَّ الإِذْخِرُ».

Maana yake, “Allah amepatukuza Makka. Hairuhusiwi kuokota vitu vyake (vilivyodondoka), wala miti yake isikatwe, wala wanyama wake wasiwindwe, na wala majani yake yasikatwe”. Akasema Ami ya Al`Abbaas, “Isipokuwa Al Idhkhira Ewe Mtume S.A.W”, Akamjibu, “Isipokuwa Al Idhikhira” 

Arrabi`i kasema, " الإِذْخِرُ(Al Idhkhira), ni aina fulani ya mimea ambayo ilikuwa ikifanyiwa mikeka, au majamvi, na kuezekewa nyumba.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment