Ibadhi.com

1. FARIDHA YA HIJA.

 

 

392. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Al-Fadhlu Ibnul Abbas alikuwa kamkwea mnyama nyuma ya Mjumbe wa Allah (S.A.W.), akaja mwanamke wa kabila la Khash`am kuuliza masuala ya kidini. Al-Fadhlu Ibnul Abbas (R.A.A.) akawa anamwangalia (yule mwanamke), naye yule mwanamke anamuangalia (yaani wanaangaliana). Mjumbe wa Allah (S.A.W.) akauzungusha uso wa Al-Fadhl upande mwingine. Yule mwanamke akauliza akasema, "Ewe Mjumbe wa Allah, ninajua kwamba Hija ni faridha ya Allah kwa waja Wake, baba yangu ni mzee sana, hamudu kujithibitisha (hawezi kukaa) sawa sawa kwenye kipando cha usafiri, jee ninaruhusiwa kumhijia?” Akasema, "

 

«أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أَبِيكِ دَيْنٌ فَقَضَيْتِهِ عَنْهُ، أَكُنْتِ قَاضِيَةً عَنْهُ؟»

 

Maana yake, “Unaonaje lau kama baba yako angelikuwa na deni ukamlipia basi jee, si ungalikua umemlipia?” Akajibu akasema, "Naam ningelimlipia”.  Akasema Mjumbe wa Allah (S.A.W.), "

 

«فَذَاكِ ذَاكِ».

 

Maana yake, “Hivi ndivyo ufanye kama hivyo”.

 

 

 

393. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mjumbe wa Allah (S.A.W.) hakuhiji ila baada ya hija kumi baada ya Hijra yake (safari yake ya kuhamia Madina), wala hakumkana[1] asiyekwenda kuhiji katika watu wake (umma wake).

 

 

 

394. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A) kasema, " Maana yake, “Siku moja Mtume wa Mola (S.A.W.) alisali (Sala ya) adhuhuri akakaa akasema, "

 

«سَلُونِي عَمَّا شِئْتُمْ وَلاَ يَسْأَلَنِي أَحَدٌ مِنْكُمْ عَنْ شَيْءٍ إِلاَّ أَخْبَرْتُهُ بِهِ»

 

Maana yake, “Niulizeni mnachotaka, wala haniulizi mmoja wenu chochote kile isipokuwa nitamwelezea”. L-Aqraa Ibn Haabis akasema, "Ewe Mjumbe wa Allah jee Hija ni wajibu (faradhi) kwetu sisi kila mwaka?” Akakasirika Mtume wa Allah (S.A.W.) hadi mashavu yake mawili yakawa mekundu kisha akasema, "   

 

«وَالذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ قُلْتُ نَعَمْ، لَوَجَبَتْ، وَلَوْ وَجَبَتْ لَمْ تَفْعَلُوا، وَلَوْ لَمْ تَفْعَلُوا لَكَفَرْتُمْ، وَلَكِنْ إِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَيْءٍ فَانْتَهُوا، وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَيْءٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ».

 

Maana yake, “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko mkononi Kwake. Ningelisema ndiyo, ingeliwawajibikia. Na ingeliwajibikia msingalifanya. Na kama msingalifanya mngelikufuru. Lakini nikikukatazeni kitu acheni. Na nikikuamrisheni kitu kifanyeni kwa kadri ya uwezo wenu”.

 

 

 

395. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kasema, "Mtu mmoja alikuja kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.) akasema kumueleza Mtume (S.A.W.), “Ewe Mtume wa Allah hakika mama yangu ni mzee sana, na siwezi kumpandisha juu ya ngamia, na nikimfunga namkhofia asije akafariki dunia, jee nimhijie?” akasema, "

 

«نَعَمْ».

 

Maana yake, “Ndiyo”. 

 [1] Kumkemea au kumlaumu.

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment