Ibadhi.com

10. USHIRIKINA NA UKAFIRI.

 

59.Abu Ubaydah, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Anas Bin Maalik (R.A.A.), kutoka kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«مَنْ أَشْرَكَ سَاعَةً أُحْبِطَ عَمَلُهُ، فَإِنْ تَابَ جُدِّدَ لَهُ الْعَمَلُ».

Maana yake, “Mwenye kushirikisha kwa muda mchahe tu, vitendo (thawabu) zake huporomoshwa (vinaharibika), akitubu amali zake hurejeshewa”.

 

60. Abu Ubaydah, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.), kutoka kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«يَقُولُ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى مَنْ عَمِلَ عَمَلاً أَشْرَكَ فِيهِ غَيْرِي فَهُوَ لَهُ كُلُّهُ، وَأَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ».

Maana yake, “Anasema Allah aliyetukuka, na mwingi wa utukufu, "Mwenye kufanya kitendo akamshirikisha mwingine asiyekuwa Mimi, basi vyote atarejeshewa mwenyewe (yaani hapati thawabu yoyote ndani yake). Na Mimi najitosheleza sihitajii mshirika”.

 

61. Abu Ubaydah, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Aisha (R.A.A.H). mke wa Mtume wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«مَنْ زَعَمَ أَنَّ مُحَمَّدًا رَأَى رَبَّهُ فَقَدْ أَعْظَمَ عَلَى اللَّهِ الْفِرْيَةَ».

Maana yake, “Mwenye kudai (kusema) kwamba Muhammad (S.A.W.) alimuona Mola wake, basi amemsingizia Allah uongo mkubwa”.

 

62. Abu Ubaydah, kutoka kwa Jaabir bin Zayd kasema, "Imenifikia kutoka kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.), kwamba alisali pamoja na Sahaba zake Sala ya asubuhi akiwa L-Hudaybiya, na athari ya mvua ilionyesha usiku ilikuwa bado iko katika mawingu, alipotoka (alipomaliza) kutoka kwenye Sala yake akawageukia watu akasema, "

«هَلْ تَدْرُونَ مَا قَالَ رَبُّكُمْ؟» قَالُوا: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «قَالَ: أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ بِالْكَوَاكِبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي وَمُؤْمِنٌ بِالْكَوَاكِبِ».

Maana yake, “Jee mnafahamu nini kasema Mola wenu?” Wakasema, “Allah na Mjumbe wake ni wajuzi zaidi”. Akasema, “Kasema, "Wamepambazukiwa na asubuhi waja wangu waumini, na makafiri, ama yule atakaesema tumeteremshiwa mvua kwa fadhila za Mola na rehema Zake, huyo ni mwenye kuamini, na kazikufuru nyota, ama atakaesema kuwa tumeteremshiwa mvua kwa kunasibisha (kuhusisha) kwa nyota hii na hii, basi amenikufuru mimi na kuamini nyota”.

 

63. Kasema Ar-Rabi`I, "Kasema Abu Ubaydah, “Nimepata habari kutoka kwa Mtume wa Allah (S.A.W.) kuwa kasema, "

«إِنْ كَانَ زَيْدُ بْنُ عَمْرٍو لأَوَّلَ مَنْ عَابَ عَلَيَّ عِبَادَةَ الأَصْنَامِ وَالذَّبْحَ عَلَيْهَا، وَذَلِكَ أَنِّي أَقْبَلْتُ مِنَ الطَّائِفِ وَمَعِي زَيْدُ بْنُ حَارِثَةَ، وَمَعَنَا خُبْزَةٌ وَلَحْمٌ، وَكَانَتْ قُرَيْشٌ آذَتْ زَيْدَ بْنَ عَمْرٍو حَتَّى خَرَجَ مِنْ بَيْنِ أَظْهُرِنَا، فَمَرَرْتُ بِهِ وَعَرَضْتُ عَلَيْهِ السُّفْرَةَ، فَقَالَ: يَا ابْنَ أَخِي أَنْتُمْ تَذْبَحُونَ عَلَى أَصْنَامِكُمْ هَذِهِ؟ فَقُلْتُ: نَعَمْ، فَقَالَ: لاَ آكُلُهَا، ثُمَّ عَابَ الأَصْنَامَ وَالأَوْثَانَ وَمَنْ يُطْعِمُهَا وَمَنْ يَدْنُو مِنْهَا. قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَاللَّهِ مَا دَنَوْتُ مِنَ الأَصْنَامِ شَيْئًا حَتَّى أَكْرَمَنِي اللَّهُ بِالنُّبُوَّةِ»

Maana yake, “Kwa hakika Zayd bin Amru alikuwa ni wa kwanza kunielezea ubaya wa kuabudu masanamu, na kuwachinjia, aliyasema hayo nilipokuwa natoka Taif pamoja na Zayd Bin Haaritha, na tulikuwa na mkate na nyama. Maquraishi walikua wamemuudhi Zayd bin Amru mpaka ikampelekea kuondoka miongoni mwetu (yaani akajitenga pekee yake), nikampitia na nikampa chakula, akasema, "Ewe mtoto wa ndugu yangu!, Nyinyi mnachinja kwenye masanamu yenu haya?[1], Nikasema, “Ndio[2]”. Akasema, “Sitokula”.  Kisha akasema maneno mabaya kuhusu hayo masanamu, na mwenye kuyalisha, na anaye yakurubia. Akasema Mjumbe wa Allah (S.A.W.), “Ninaapa kwa Mola sijapata kuyakurubia kabisa masanamu kwa kitu chochote kile, mpaka Allah aliponikirimu kwa Utume (yaani katu hakuwahi kuyakurubia)”. Kasema, “Alipewa utume akiwa na umri wa miaka arubaini, na alikaa na Israfiil (A.S.) miaka mitatu, na hapana kitu kilichoteremshwa, halafu akaondoka Israfiil akakaa na Jibriil (A.S.), Mola akamteremshia Qur-ani miaka kumi akiwa Makka, na miaka kumi akiwa Madina. Na alifariki akiwa na umri wa miaka sitini na tatu”.

 

64. Abu Ubaydah, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.A.) kasema," Kasema Mjumbe wa Allah (S.A.W.), "

«رَأْسُ الْكُفْرِ نَحْوَ الْمَشْرِقِ، وَالْفَخْرُ وَالْخُيَلاَءُ فِي أَهْلِ الْخَيْلِ وَالإِبِلِ، وَالْجَهْلُ فِي الْفَدَّادِينَ أَهْلِ الْوَبَرِ، وَالسَّكِينَةُ فِي أَهْلِ الْغَنَمِ».

Maana yake, “Kichwa cha ukafiri upande wa mashariki, na ufakhari, na kiburi, kwa wenye farasi, na wenye ngamia, na ujahili, ni kwa wachungaji wa wanyama wanaochunga kwa sauti za makelele, na utulivu, na unyenyekevu kwa watu wenye mbuzi”.

 

65. Abu Ubaydah, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.), kutoka kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«مَنْ قَالَ لأَخِيهِ: يَا كَافِرُ، فَقَالَ لَهُ: أَنْتَ الْكَافِرُ فَقَدْ بَاءَ بِالْكُفْرِ أَحَدُهُمَا، وَالْبَادِئُ أَظْلَمُ».

Maana yake, “Mwenye kumwambia ndugu yake (Muislamu) “Ewe kafiri!” Naye akamwambia, “Wewe kafiri,” basi unamrudia ukafiri mmoja wao, na aliyeanza ni dhalimu zaidi”.

 

66. Abu Ubaydah kasema, "Imenifikia kutoka kwa Mjumbe wa Allah (S.A.W.) kasema, "

«الرِّيَاءُ يُحْبِطُ الْعَمَلَ كَمَا يُحْبِطُهُ الشِّرْكُ».

Maana yake, “Ria[3] kuna haribu (thawabu za) vitendo, kama vile unavyo haribu ushirikina”.[1] Inakusudiwa watu wake.

[2] Inaweza kuwa kajibu hivyo ili ajue kutoka kwake anayoyafahamu yeye kuhusu kuchinjia masanamu, sio kama Yeye amekubali kuwa alikuwa akichinjia masanamu.

[3] Kufanya jambo kwa ajili ya kutaka kuonekana au kusifiwa na watu, kujionesha.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment