Ibadhi.com

52. UHUSIANO WETU NA MASAHABA R.A.

Asalamu alykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Allah ameridhia kwetu kufuata Assaabiquna Al-Awwaluun (Masahaba wa mwanzo waliotangulia) katika Muhajirina na Ansaar, jee! kupitia itikadi yenu Maibadhi -bila kurefusha- munaweza kutueleza fungamano lenu na Masahaba hawa kwa kuchukua kutoka kwao na kwa fahamu yao?

JAWABU

Kusifiwa Masahaba -Allah mtukufu awaridhie- ni kwa sababu ya kuukubali Uislamu kwa kufuata maamrisho yake na kuepuka makatazo yake na kuyaenzi mafundisho yake, kwa hiyo Masahaba wa mwanzo Waliotangulia katika nini? Bila shaka ni katika kumtii Allah na Mtume wake S.A.W. na waliowafuata Masahaba hao katika nini? Bila shaka ni katika kumtii Allah na Mtume wake S.A.W. na hilo ndilo fungamano kuu linalotukusanya sisi na wao, unatukusanya Uchamungu na utiifu wa kumtii Allah mtukufu na Mtume wetu S.A.W., inatukusanya Itikadi isiyokubali kuwapendela Mafasiki na Madhalimu, inatukusanya Quraani tukufu.

Kutokana na hapo yoyote anayejitoa nje ya utiifu wa Allah na Mtume wake baada ya kuamini kwake huyo hayumo katika maridhio ya Allah mtukufu isipokua kama atatubia.

Wallahu aalamu.

Wabillahi taufiqi.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment