Ibadhi.com

51. NI IPI HUKUMU YA MASHIA?

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Tunataka kujua ni ipi hukumu ya Mashia kwa mujibu wa mafundisho ya Ibadhi?

JAWABU:

Mashia wamegawika lakini wote wanakusanyika katika kumnyanyua daraja Imam Ali bin Abi Talib R.A. zaidi ya Masahaba wote, ni wengi wao -kama si wote- wanaitakidi kuwa Imam Ali ni maasuum -yaani amehifadhika na kufanya kosa-, na hapa ndipo tunapowaona kupotea kwao, kwa sababu makosa yalipatikana kwa Imam Ali bin Abi Talib pale alipokubalia wito wa Tahkiim uliotoka kwa Muawiyah bin Abi Sufiyan na kundi lake ambalo hakuna shaka yoyote kuwa ni kundi la waasi kwani ndilo lililomuua Ammaar bin Yaasir R.A. na Mtume S.A.W. amesema: ((Ammaar atauliwa na kundi la waasi)), na wito huo wa Tahkiim ulimuingiza Imam Ali katika makosa ya kuvunja hukumu ya Allah tukufu ya kulipiga vita kundi la waasi hadi lirejee katika amri ya Allah ambayo kwa kuasi kwao amri hiyo umepatikana uasi wao na wakastahiki kupigwa vita, pia kosa la kumthibitisha Muawiyah katika uadui dhidi ya Ukhalifa ambao ni amana katika mikono ya Ali bin Abi Talib, na hayo ndiyo yaliyowapelekea Salafu wetu wema Ahalu Naharawani -Allah awaridhie- kujitoa katika safu ya Imam Ali; kwani waliona kubakia katika safu yake ni kusadia katika dhambi na uadui nako kumekatazwa na Allah mtukufu, pia ni kuingia katika utiifu wa kiumbe kwa kumuasi Muumba, nako pia kumekatazwa katika Uislamu, kwa hiyo wakaiacha safu yake na kujichagulia Kiongozi kwa njia ya Shuuraa naye ni Imam Abdullahi bin Wahbi Al-Raasibi R.A. kisha wakajichagulia mji wa Naharawani ambapo baada ya Imam Ali kupinga matokeo ya Tahkiim baina yake na Muawiyah akafanya kosa jengine la kuwapiga vita Ahalu Nahrawani kiuadui na dhulma, na baada ya hapo hakuweza tena kuelekeana na Muawiyah, na Ukhalifa ukaanguka kwa makosa hayo yaliyotokezea, na hapo ukaanza Utawala wa Bani Umayyah ambao haukujua njia ya uadilifu wala huruma, wakabakia Mashia ni wenye misiba ya Hussein ya kuomboleza kusikomalizika, na wakaingia katika mkondo wa kutukana ovyo Masahaba wa Mtume S.A.W. bila ya haki, na kuwalengea tuhumahewa Wake wa Mtume S.A.W. Mamama wa Waumini Bi Aisha Bi Hafsa Allah awaridhie , na wakaleta katika dini yao mambo ya ajabu ajabu ambayo hayana nafasi katika Uislamu.

Juu ya yote hayo Maulamaa wetu hawajawatoa Mashia nje ya Uislamu, ingawa wamewaona kuwa ni wapotevu na wabatilifu.

Amesema Sheikh Abu Bakar Ahmed Al-Kindi r.a.:

وعلى من جاحد هذه القاهدة فارق المسلون الروافضَ وخالفوهم، وشهدوا عليهم بالكفر كفر نفاق لا كفر شرك؛ إذ هم مخطؤون في التأويل لا التنزيل؛ ونحن من جميع أولئك براء وبالله التوفيق.

"Na kwa sababu ya kupinga msingi huu, Waislamu wamejitenga na Maraafidha (Mashia wapingaji wa Ukhalifa wa asiyekua Ali bin Abi Talib na kizazi chake) na wakatafautiana nao, na wakawashudia kwa ukafiri, ni ukafiri wa kinafiki si ukafiri wa kishirikina; kwani wao wamekosea katika taawili na sio katika tanziili, na sisi tunajitenga na wote hao. Na taufiqi ni ya Allah." [Jauhar Muqtassir 133]

Wallahu aalamu.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment