Ibadhi.com

50. HAKUNA KATIKA NYINYI ILA ATAUINGIA TU

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Anasema Allah mtukufu katika Suuratu Maryam:

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا * ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا

((Na hakuna yoyote katika nyinyi ila atauingia, limekua hilo kwa Mola wako ni pitisho imeshapitishwa * kisha tutawaokoa wale waliomcha Allah na tutawaacha Madhalimu humo wakiyayatika)) [Maryam 71-72]

Jee! Waislamu wataingia Motoni pamoja na Madhalimu kisha watatolewa?

JAWABU:

Bila shaka adhabu ya akhera inawahusu Makafiri peke yao, ni sawa ukafiri wao uwe wa kishirikina ambao unawahusu Washirikina, au uwe ukafiri wa neema wa kinafiki ambao unawahusu Waislamu Mafasiki waliokufa bila kutubia, wote hao ukafiri umewakusanya kama ulivyowakusanya ufasiki na udhalimu.

Ama Waislamu Wachamungu wao siku hiyo ya Kiama watakua katika amani kamili hawafikwi na khofu wala huzuni yoyote, anatuambia Allah mtukufu:

إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ * لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِي مَا اشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَالِدُونَ * لَا يَحْزُنُهُمُ الْفَزَعُ الْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ هَٰذَا يَوْمُكُمُ الَّذِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ 

((Hakika wale waliotanguliwa kupata wema utokao kwetu, wao hao wataepushwa nao (huo moto) * hawatasikia hata sauti yake, nao katika yanayotamaniwa na nafsi zao watabakia * haitawahuzunisha fazaa kuu, na watakutana na Malaika: Hii ndiyo siku yenu muliyokua mukiahidiwa)) [Al-Anbiyaa 101-103]

Vilevile Allah mtukufu anatuambia:

يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ 

((siku ambayo Allah hatawadhalilisha Nabii na walioamini pamoja naye)) [Tahriim 8]

Na yeye ametuambia kupitia ndimi za waja wake wema:

رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

((Ewe Mola wetu hakika wewe yule utakaemuingiza Motoni kwa hakika huyo umemdhalilisha, na Madhalimu hawana kabisa wa kuwanusuru)) [Aala Imraana 192]

Ama kuhusu Aya za Suuratu Maryam Allah mtukufu anatueleza katika sura hiyo hiyo:

يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَٰنِ وَفْدًا * وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا 

((Siku tutakapowakusanya wachamungu wakiwa kwa Allah ni wakirimiwa * na tutawapeleka waovu katika Jahannamu kuiingia)) [Maryam 85-86]

Kwa hiyo wachamungu ni wakirimiwa wa Allah hivi atawakirimu kwa kuwaingiza Motoni? Hapana kisha hapana, bali atawakirimu kwa amani iliyotimia na mazuri ya kufurahisha nafsi zao.

Kutokana na hapo, pale Allah aliposema:

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا * ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا

((Na hakuna yoyote katika nyinyi ila (huo moto) atauingia, limekua hilo kwa Mola wako ni pitisho imeshapitishwa * kisha tutawaepusha Wachamungu na tutawaacha Madhalimu humo wakiyayatika)) [Maryam 71-72]

alikua anawambia wakusudiwa maalumu kwa namna ya kuwageukia (Al-Iltifaatu) na wakusudiwa hao ni wapinga ufufuo wa Akhera anatumbia Allah amtukufu:

وَيَقُولُ الْإِنسَانُ أَإِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا * أَوَلَا يَذْكُرُ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْئًا * فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا * ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَٰنِ عِتِيًّا * ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا 

((Na Mtu anasema: Hivi nikishakufa kweli nitatolewa nikiwa hai? * Hivi hakumbuki (huyu) Mtu hakika sisi tulimuumba hapo kabla wala hukua kitu?!! * Kwa haki ya Mola wako kwa hakika hasa tutawakusanya na mashetani kisha tutawahudhurisha pembezoni mwa Jahannamu wakiwa tako * kisha tutavua katokana na kila kundi walio wakaidi zaidi mbele ya Mrehemevu * kisha sisi hasa tunajua zaidi wale ambao wanastahiki huo (Moto) kuuingia)) [Maryam 66-70]

Kisha hapo ndio anawageukia hao wahusika wanaostahiki adhabu ya Motoni na kuwambia:

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا * ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا

((Na hakuna yoyote katika nyinyi ila atauingia, limekua hilo kwa Mola wako ni pitisho imeshapitishwa * kisha tutawaepusha Wachamungu na tutawaacha Madhalimu humo wakiyayatika)) [Maryam 71-72]

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment