Ibadhi.com

2. TAFSIRI YA JUMLATU TAUHIDI

Jumla ya Tauhidi ndio mkusanyo wa dini yote ya Uislamu, basi tujuwe kuwa Jumla ya Tauhidi hii inayo tafsiri yake ambayo imesimama katika misingi ya kusimama hoja na dalili katika kulazimika ambayo yatalazimika kwa mja, basi tufahamu kuwa yako yale ambayo mja anayo dharura ya kuwa mjinga ndani yake nayo ni yale yote ambayo hoja na dalili ya kulazimika wake haijasimama juu yake, na yako ambayo mja hana dharura ya kuwa mjinga ndani yake nayo ni yale ambayo hoja ya kulazimika kwake imesimama juu yake, basi kila ambalo mja hajuwi ulazima wake ujinga wake wa jambo hilo hautakuwa na nafasi baada ya kusimama hoja ya kulazimika kwake.

Basi tafsiri ya jumla ya tauhidi imegawika aina mbili kuu, nazo ni:

1. TAFSIRI YA KIITIKADI:

Nayo inakamatana na yale yaliyolazimika kuyaitakidi mja moyoni mwake, nayo hayo huwa ndio mwangaza wa Imani katika maisha yake, kwa hiyo kila lenye kulazimika kiitikadi kwa kulithibitisha au kulikanusha hilo huingia katika Tafsiri ya Jumlatu Tauhidi Kiitikadi, nayo ndiyo maudhui ya Itikadi (aqidah) sahihi.

2. TAFSIRI YA KIMATENDO:

Nayo inakamatana na matendo ya dhahiri, nayo ni matendo ya viungo vya mja katika kufanya au kuepuka, ni sawa matendo haya yakawa ni matamko ya ulimini, au tabia katika jamii, au vitendo vya Ibada maalumu za kutekeleza Amri au kuepuka Katazo.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment