Ibadhi.com

1. JUMLATU TAUHIDI (SHAHADA)

Inalazimika kwa kila ileyefikia baleghe (utu uzima) na akawa na akili ashuhudie kuwa:

﴿لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًّا عَبْدُهُ وَرَسُوْلُهُ، وأَنَّ مَا جَاءَ بِهِ مُحَمَّدٌّ حَقٌّ مِنْ عِنْدِ اللهِ﴾

Hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah, na kuwa Muhammad ni mja wake na mtume wake, na kuwa yale aliyokuja nayo Muhammad ni haki inayotoka kwa Allah﴿

Na hii ndio Jumla ya Tauhidi aliyokuwa Mtume wa Allah (s.a.w) akiilingania kwa waja, basi yoyote atakayeikubali Jumla hiyo huyo atakuwa ni muumini kipenzi (Walii), ikiwa tu hakijalazimika kwake kitu chochote katika tafsiri ya jumla kiitikadi, au kimaneno, au kimatendo, na yeye ataendelea kuwa ni kipenzi wa waumini - baada ya kulazimikiwa na hiyo tafsiri - ikiwa hatoipuuza tafsiri hiyo, kwa kuwacha lililolazimika kiitikadi, kimatendo na kitabia, au kwa akafanya lililoharamishwa.

 

DALILI YA JUMLATU TAUHIDI

Amesema Allah mtukufu:

(فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنْزَلْنَا ۚ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ)

((Basi muaminini Allah na Mtume wake na Nuru ambayo tumeiteremsha, na Allah kwa munayofanya ni mwenye kuyajua vuzuri)).

[Surat At-Taghabun 8]

Kwa hiyo tumeamrishwa kuamini mambo matatu nayo ndiyo yale yaliyokusanywa katika Jumlatu Tauhidi:

1. Kumuamini Allah (Hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah).

2. Kumuamini Mtume wa wake  ((Muhammad ni mja wa Allah na mtume wake)).

3. Kuamini Nuru aliyoiteremsha Allah (yale aliyokuja nayo Muhammad ni haki inayotoka kwa Allah).

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment