Ibadhi.com

18. KULAANIANA MUME NA MKE

 

Ikiwa mume atamtuhumu mke wake kwa kosa la uzinifu, au kwa kukataa mtoto([1]), na hali hana mashahidi wanaokubalika katika hilo, basi italazimika kulaaniana na mke wake iwapo mwanamke atakataa kuhusika na kosa hilo.

﴿وَٱلَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوٰجَهُمْ وَلَمْ يَكُنْ لَّهُمْ شُهَدَاء إِلاَّ أَنفُسُهُمْ فَشَهَـٰدَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَـٰدَاتٍ بِٱللَّهِ إِنَّهُ لَمِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ * وَٱلْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَةَ ٱللَّهِ عَلَيْهِ إِن كَانَ مِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ * وَيَدْرَؤُاْ عَنْهَا ٱلْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِٱللَّهِ إِنَّهُ لَمِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ * وَٱلْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ ٱللَّهِ عَلَيْهَا إِن كَانَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ﴾

Na wale wanaowalengea (kosa la uzinifu) wake zao, na ikawa hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao wenyewe, basi ni kushuhudia mmoja wao kwa mashuhudio manne ya kuapa kwa Allah kuwa yeye ni katika wakweli * na shuhudio la tano ya kuwa laana za Allah ziwe juu yake ikiwa yeye ni katika waongo * Na itamwondokea (mwanamke) adhabu kwa kushuhudia mashuhudio manne ya kuapa kwa Allah kuwa huyo (mume wake) ni katika waongo * na shuhudio la tano ya kuwa Makasiriko ya Allah yawe juu yake (huyo mke) ikiwa yeye (mume) ni katika wakweli﴿ [Nuur 24/06-09]

Wakilaaniana mume na mke basi ndoa inavunjika baina yao, na haihesabiwi kuwa ni talaka, na ndoa haitowakusanya tena  baina yao milele, hayo ni kwa sababu ya yale yaliyothibiti kuwa Mtume (s.a.w) alimtenganisha mume aliyemtupia mke wake kosa la uzinifu, basi baada ya kulaaniana baina yao, kama alivyoamrisha Allah mtukufu; Mtume (s.a.w) akasema:

"إِنَّهُمَا لاَ يَجْتَمِعَانِ أَبَداً"

"Hakika hao wawili hawatokutana tena milele (yaani kindoa)”

[Rejea: Rabii 606, Muslim 1492: 2, 3, Bukhari 5306, 5311][1]. Imekuja kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema: ((Mwanamke yoyote atakayeingiza katika watu asiyekuwemo katika wao, basi hana kitu kwa Allah,  na hatoingizwa  na Allah katika pepo, na mwanamme yoyote akimkataa mtoto wake na yeye anamuona, basi Allah atamfungia rehma zake, na atamfedhehesha juu ya vichwa vya viumbe kuwanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho)) [Al-hakim 2868], Na mwanamke kuingiza katika watu asiyekuwemo yaani amechukuwa mimba kwa uzinifu na hali anaye mume, basi akaingizia katika familia ya bwana wake asiyekuwa wake, na mwanamme anayekataa mtoto wake, yaani ameowa mke wake kisha akamzalia mtoto, na huyo Bwana akakataa huyo mtoto, na hali hana yakini kuwa mtoto sio wake.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment