Ibadhi.com

16. TAWAFU YA IFADHA NA SA'YI

 

Tawafu ya ifadha ni moja kati ya nguzo za hija; hija huharibika kwa kuiacha.

Ni katika sunna kutekeleza mawili haya siku ya tarehe 10 Dhul-hija baada ya kupiga jamra, kuchinja na kunyoa au kupunguza nywele, lakini inajuzu kuyaakhirisha japo baada ya siku za tashriq.

Mwenye hedhi ataakhirisha tawafu ya ifadha mpaka atahirike.

Baada ya kutekeleza mawili haya inakuwa halali kwa mwenye kuhiji kila alichokuwa kazuiliwa isipokuwa kuwinda kwenye eneo la Haram; na hali hii huitwa “tahal-lul akbar” yaani kutokana na ihramu kukubwa.

 

 

MAZINGATIO

Atakayetufu tawafu ya ifadha kisha akalala Maka mchana na kurejea Mina jioni hapana kitu juu yake lakini amefanya kinyume na lililo bora.

Haizuiwi kula na kunywa Maka baada ya tawafu ya ifadha, ila imekataliwa kulala hapo mchana, lakini linalotegemewa katika fatwa ni kuwa inajuzu kulala mchana kwa vile imethibiti kuwa Mtume - rehma za Allah na amani zimshukie - alilala mchana baada ya kutufu.

Aliyetufu tawafu ya ifadha mizunguko sita akakumbuka baada ya kurejea nchini kwake itamlazimu arudi kwenye Haram na arudie tawafu ya ufadha katika mwaka wake huo, na hapana kitu juu yake kwa rai ya baadhi ya wanazuoni ikiwa hajamuingilia mkewe; ama ikiwa vinginevyo basi hana budi kuhiji tena.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment