Ibadhi.com

12. HUKUMU ZA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 10 DHUL-HIJA

 

¨     Kulala Muzdalafa baada kuondoka Arafaat.

¨     Katika sunna ni kuchanganya sala mbili: ya magharibi na isha huko Muzdalafa kutokana na hadithi ya Mtume - rehma za Allah na amani zimshukie: “Kuwa yeye - rehma za Allah na amani zimshukie - alifika Muzdalafa akachanganya magharibi na isha kwa adhana moja na iqama mbili na hakusali cho chote baina yao.”[1]

¨     Muzdalafa yote ni pa kusimama isipokuwa ‘Waadi Muhas-sir’, kutokana na kauli yake - rehma za Allah na amani zimshukie: “Muzdalafa yote ni pa kusimama na msikae kwenye Muhas-sir.” Imepokewa na Ahmad. Muhas-sir ni njia ya maji bina ya Muzdalafa na Mina na ni karibu zaidi na Muzdalafa (ni eneo alipofikwa na adhabu Abraha).

¨     Imeruhusiwa kwa wanawake, watoto na wachungaji kuondoka Muzdalafa usiku baada ya kutua kwa mwezi[2].

¨     Inapasa kulivuka bonde la Muhas-sir kabla kuchomoza kwa jua ila kwa dharura.

¨     Kuomba dua kwenye ‘Al-mash-ar Al-haraam’ (Muzdalafa) ni wajibu, na inatosheleza dua yo yote au kutamka ‘Laa ilaha illa LLah’ au kuhimidi au kutamka talbia. Akifanya lo lote kati ya hayo wajibu umeshamuondokea.

 

MAZINGATIO

·        Walio dhaifu na wenye udhuru wameruhusiwa kuondoka Muzdalafa baada ya nusu ya usiku.

·        Mwenye kuhiji ajitahidi kufika Muzdalafa hasa pakiwa na zahama; asipowahi kukaa usiku huko kwa sababu hiyo hapana kitu juu yake.

·        Akikhofia wakati wa sala kumfutu akiwa njiani kuelekea Muzdalafa atasali pahala alipo.[1] - Ameipokea a'Nasai, Abu Daud, Ibnu Maajah na Ibnu Abi Shaiba.

[2] - Kwa mujibu wa wenye ilmu, rukhsa hii pia ni kwa kila aliye dhaifu.(Mfasiri)

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment