Ibadhi.com

9. KUTOKANA NA IHRAMU YA UMRA

 

·        Akimaliza mwenye kufanya umra sa'yi yake atanyoa au kupunguza nywele zake. Kunyoa ni bora kuliko kupunguza, na izingatiwe kwamba kupunguza lazima kuenee kichwa chote. Ama mwanamke atapunguza nywele zake nchani kadiri ya urefu wa ncha ya kidole kuanzia kiungo cha juu.

·        Baada ya kunyoa au kupunguza nywele atakuwa ameshatokana na ihramu yake akiwa mfanya Tamat-tu'. Ama akiwa mfanya Qiraanu hatanyoa ila siku ya kuchinja kule Mina.

·        Yanamhalalikia mwenye kufanya umra baada ya kutokana na ihramu kila yanayomharamikia muhrimu isipokuwa kuwinda katika Eneo Takatifu (Al-Haram).

·        Mfanya Tamat-tu' bora kwake kupunguza nywele baada ya kufanya umra, na kunyoa baada ya kulipiga Jamra Kuu la Aqaba na kuchinja ikiwa nywele zake fupi baina ya umra na hija.

 

MAZINGATIO

¡  Hakatazwi mtu kujinyoa au kujipunguza nywele mwenyewe kwa ajili ya kutokana na ihramu, lakini inachukiwa kufanya hivyo uchukivu wa kiutakaso akiwapo wa kumfanyia hayo kati ya wasio wahirimu.

¡  Hazuiwi muhrimu kumnyoa au kumpunguza nywele muhrimu mwengine, kwani hapana dalili ya kuzuia, na kuzuia hili kutaleta usumbufu mkubwa, lakini bora yule ambaye ameshatokana na ihramu amtoe katika ihramu aliye muhrimu.

¡  Mwenye kutanguliza kunyoa kabla ya kuchinja na kupiga Jamra, kuna kauli kuwa atayefanya hivyo kwa sahau au kuto kujua hana kosa, na kauli hii ndiyo inayofuatwa katika fatwa, na kuna kauli kuwa atayefanya lo lote kati ya hayo atalazimika kuchinja.

¡  Halitoshi wanalofanya wengi kati ya watu zama hizi - la kukata nywele kidogo kwa mwanamme, bali wajibu kupunguza sehemu zote za nywele mpaka ijulikane kuwa mtu huyo amepunguza nywele zake.

¡  Haisihi kwa mfanya Tamat-tu' kutokana na ihramu yake ya hija kabla ya kuchinja mnyama wake. Ikiwa hakuweza kuchinja siku ya kuchinja (10 Dhulhija) atabaki na ihramu yake mpaka achinje.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment