Logo
Print this page

3. KUSAFIRI KWA MDAIWA KWENDA HIJA AU UMRA

 

 Anayedaiwa anatakiwa atokane na deni analodaiwa ili aje kwa Allah akiwa ametakasika na kila jukumu. Likishindikana kwake hilo, asiondoke ila wakimruhusu wanaomdai bila ya kuwataka muhali katika kuwaomba wamruhusu, na ausie madeni wanayomdai. Haya iwapo deni umefika wakati wake wa kulipwa.

 Ama ikiwa haujafika wakati wake wa kulipwa, itamjuzia kuondoka bila ruhusa yao kwa sharti ausie wanachomdai. Na haya kwa hali yo yote ni kwa yule aliye nacho cha kulipa; ama asiyekuwa na cha kulipa asiondoke kwenda hija mpaka atokane na kila deni analodaiwa, na Allah ni Aula wa kuukubali udhuru wake.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
All Rights Reserved.