Ibadhi.com

JIMAA SIKU ZA HEDHI

Tambua Ewe Mwanafunzi, Allah akurehemu kuwa haifai kumuingilia mwanamke katika siku zake, Allah katukataza vikali, na akatuambia ni uchafu kufanya hivyo. Naam, anayo haki Mume kujistarehesha na Mkewe siku za hedhi anavyotaka ispokuwa ajiepushe na tendo la ndoa, Mtume (s.a.w.w.) amesema: ((Fanyeni kila kitu ispokuwa Jimaa))[1].

ASIESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU

Sasa Mtu akaja-akafanya vitimbi vyake mpaka akaingia huko alikokatazwa na Mola wake, hapo itambidi: ((Atoe Sadaka ya Dinari moja ya dhahabu ikiwa ni katika siku za mwanzo-mwanzo za hedhi, na Nusu-dinari ya dhahabu ikiwa ni katika siku za mwisho-mwisho za hedhi))[2], Dinari moja ni sawa na Gramu 4.25, na Nusu dinari ni sawa na 2.125gm, kasha atubie, ajute na akome kuasi makatazo ya Allah, wala asije akadhani kuwa vipesa vyake ndio vitakavyomruhusu kwenda kinyume na makatazo hayo kila akitaka kufanya ukhabithi wake, Hapana, tena hapana mara elfu! Wallaahu-A'alam.

---------------------------------------------------------

[1]-  Hadithi Sahihi, amesahihisha Muslim (1/16 (246), Ahmed (3/132 (246), Abu-Daaud (1/67 (258) kutoka kwa Anas bin Malik (r.a) Marfuu’an.

[2]-  Dinari 20 ni sawa na 85gm, kwa hivyo Dinari Moja ni sawa na 4.25gm, na Nusu dinari ni sawa na 2.125gm, hapa utatoa uzito huo wa dhahabu uumpe Maskini anayestahiki, au utakwenda kwa Sonara umuulize uzito huu una thamani gani, na hiyo thamani ndio utaitasaddak… Kwa mfano ukiambiwa kuwa gramu moja ni ShT. 12,000 basi utakubidi utoe Sh. 51,000 au Nusu yake 25,500 Tsh.. Kumbuka kuwa bei ya dhahabu inabadilika kila siku ima kupanda au kushuka.

 

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment