Ibadhi.com

TAN-BIHI MUHIMU KATIKA HEDHI

Tambua Ewe Mwanafunzi, Allah akurehemu kuwa Mwanamke anaweza akaona damu rangi ya manjano-manjano (rangi ya usaha), au maji yaliyokuwa kijivu-jivu (baina meusi na meupe), maji hayo yakidhihiri katika siku za hedhi yatazingatiwa kuwa ni hedhi[1], na yakidhihiri siku za tohara ya Mwanamke hayatomuingiza Mwanamke katika hedhi[2], Wallaahu-A'alam.

 

------------------------------------------------------------------------------------------

[1]-  Imepokewa kuwa wanawake walikuwa wakimpelekea Bibi Aisha mikebe, ndani mna vipamba vyenye damu ya njano-njano, naye akiwaambia: ((Msifanye haraka mpaka muone maji meupe)), na katika riwaya nyengine akisema: ((Mwanamke akiona damu basi anatakiwa aache sala, mpaka aone maji meupe kama fedha, hapo tena na aoge na asali)).. .. Riwaya hii kaipokea Maalik (1/59 (57), na Bukhaariy (Ta'aliqan) (1/420).

[2]- Imepokewa kutoka kwa Ummu-'Attiyya (r.a) kuwa amesema: ((Tulikuwa hatuoni damu ya njano, na kudra (uchafu-uchafu wa kijivu-jivu) baada ya kutoharika ni hedhi))… Riwaya hii kaipokea Abu-daaud (307), na Bukhaariy (326).

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment