Ibadhi.com

MUDA WA HEDHI

Hedhi uchache wake ni siku tatu na wingi wake ni siku kumi, kama ilivyokuja katika hadithi sahihi: ((Uchache wa Hedhi ni siku tatu, na wingi wake ni siku kumi))[1], kwa maana hiyo damu itakoyopindukia siku kumi haitakuwa tena ni Hedhi, lakini itaitwa: Istihadha, na damu hii ya Istihadha haimzuii Mwanamke kusali, wala kufunga, wala kusoma Qur-ani, wala kufanya tendo la ndoa.

------------------------------------------------------------------------------------------

[1]- Hadithi Sahihi, Kaipokea Imaam Rrabii'I katika Musnad wake (2/218 (541) kupitia kwa Anas bin Maalik, Hadithi hii imesahihishwa na Maulamaa kadha-wa-kadha kati ya hao ni Shekhe wetu Ahmed Al-Khaliliyy (r.a), Shekhe wetu Sa'iid Al-Qannubiyy, pia Imesahihishwa na Maulamaa wasiokuwa wa Kiibadhi, kama vile Sh. 'Ali Al-Qaariy katika Al-mawdhuu'aatil-kubraa, Yeye amesema kuwa: ((Hadithi hii ni Hasan)), na Sh. Abu-Ghuddaa akamuwafiki katika kuihasanisha katika sherehe yake ya kitabu: Al-manaar Al-muniif (122 (275).

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment